Habari za Punde

Dk Shein kutunuku Nishani


                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, atakabidhi nishani ya Mapinduzi kwa watu na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwa njia tofauti katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar tarehe 12 January, 1964.
Sherehe hizo zitafanyika siku ya Ijumaa  tarehe 28/3/2014 saa 10:00 alasiri na Jumamosi tarehe 29/3/2014 saa 9:30 alasiri, katika uwanja wa polisi Ziwani Zanzibar .
MWISHO.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

3 comments:

  1. nini tofauti ya nishani alizotowa Ikulu wakati wa kusherehekea miaka 50 na hizi za sasa, au ni za waliofanikisha na kuuenzi Muungano? Tupe detailed tafadhali

    ReplyDelete
  2. Details ni kuwa atawapa nishani wale watu 228 registered waliopoteza maisha yao siku ile ya tarehe 12 Januari 1964 wakiwa kama ni muhanga mpaka ikafika mimi na wewe na wengine leo hii tuko huru na tunatamba katika Zanzibar hii.Lakini mimi siwajui wakina nani hao sijui wewe mwenzangu. Au unahisi hawastahili kutunukiwa nashani???? na huenda majina yao yakaandikwa kwenye mnara wa kumbukumbu kwa wino wa dhahabu.

    ReplyDelete
  3. siamini kuwa kuna mtu Fulani ati ndio sababu ya mimi kuishi hapa kwa amani. It is in my believe that peaceful and safety I have ni kadari, rehema na neema yake ALLAH kwangu mimi. Namshukuru yeye na nitaendelea kumkumbuka yeye kwa hili. Sina haja ya kujenga mnara, kuweka nishani wala wino wa dhahabu kwa kumkumbuka mtu aliekufa kwa Mapinduzi ya nchi yeyote. Taratibuni tu nishani hizo na huo wino wa dhahabu usije kusababisha maafa na mauwaji ka wengine, maana sijui kama vijana hawatachangamkia dhahabu hizo za nje nje!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.