Habari za Punde

TASAF Yatembelea Mradi wa Mpango wa Kuondoa Umasikini katika Kaya.

Ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na washirika wa maendeleo wanaofadhili Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi uko kisiwani Zanzibar kuona namna Mpango huo unavyotekelezwa kisiwani humo. Ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea shehia ya Kijini Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja na Shehia ya Kikungwi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja ambako umezungumza na walengwa wa  mpango huo.
Wakizungumza na viongozi hao baadhi ya walengwa wameonyesha kuridhika na mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo wamesema maisha ya kaya hizo yameanza kuboreshwa huku mmoja wa walimu wa shule ya msingi Kikungwi Amrani Kombo akibainisha kuwa tangu kuanza kwa Mpango huo  mwaka jana kumekuwa na mahudhurio mazuri kwa wanafunzi kutoka katika kaya masikini ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa mpango huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mpango huo umeanza kutekelezwa kwa awamu nchini baada ya serikali kuridhia utekelezaji wake katika jitihada za kupambana na umasikini miongoni mwa wananchi. Amesema  utafiti umefanywa kwa kina kuona namna ya kuutekeleza mpango huo ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika ya maisha  ya wananchi wanajumuishwa katika mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Dkt. Idris Muslim Hijja, akizungumza na Ujumbe wa Tasaf  na Wawakilishi wa kutoka Nchi Wafadhi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa PSSN, kabla ya kuaza  kutembelea Shehia ya Kikungwi, ikiwa katika mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF mwenye suti nyeusi Ndg. Ladisilaus Mwamanga, akizungumza na kutowa maelezo katika  Ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt Idris Muslim Hijja, kabla ya kuaza kwa ziara hiyo na Ujumbe wake katika Kaya ya Shehia ya Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja. Mkoa wa Kusini.  
Mwakilisho kutoka Benki ya Dunia Bi. Ida Manjoro, akizungumza wakati walipofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kujitambulisha kwake kabla ya kuanza kwa ziara yao kutembelea Kaya Masikini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt. Idris Muslim Hijja, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa TASAF na Wawakilishi wa Maendeleo, baada ya kumaliza mazungumzo na Mkuu wa Mkoa huo, Ofisini kwake Tunguu Unguja. 
Mrattibu wa shughuli za Muungano Ndg. Iddi Silima Hassan, akitowa maelezo kwa Wananchi wa shehia ya Kikungwi wakati wa kutembelea katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini  PSSN.kikungwi.
Mwanakamatinwa Shehia ya Kikungwi wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini akisoma risala ya Wanakaya kwa Ujumbe wa Tasaf na Wawakilishi wa Ushirika wa Maendeleo wanaofadhili Mradi huo.
Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya masikini shehia ya kikungwi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, hayupo pichani akizungumza nao kuhusiana na mafanikio ya mpango huo, alipofika kutembelea Kaya hiyo Kikungwi Wilaya ya Umguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladisilaus Mwamanga, akifafanua jambo wakati wa mkutano na Walengwa na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia ya Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja.
Washirika wa Maendeleo wakiwasikiliza Wanakaya wa Shehia ya Kikungwi wakati walipofika katika shehia hiyo kujionea maendeleo ya Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika moja ya Shehia za Zanzibar,katika kijiji cha Shehia ya Kikungwi.  
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini  katika shehia ya Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF akitowa Ufafanizi baada ya kuuliza maswali Wananchi waopata Fedha kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa PSSN.
Mkurugenzi Mipango wa TASAF Ndg. Amadeus Kamagenge, akizungumza na Wananchi wa shehia ya Kikungwi wakati walipofika katika Kaya hiyo kujionea maendeleo ya Mradi wa TASAF wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini  kwa wananchi walioko katika mazingira magumu.
Mmmoja wa Mwananchi wa Shehia ya Kikungwi anayenufaika ya Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia hiyo Bi. Mwasham Muusa, akichangia katika mkutano huo ni jinsi jani ananufaika na mradi huo wa TASAF, anapata fedha kwa ajili ya kuwatunza watoto wake kulipia ada ya skuli na kumpeleka mtoto wake mwingine Kliniki kupitia mpango huo kuwatowa watoto walioko katika mazingira magumu kupata elimu. 
Mmoja wa Mlengwa wa Mradi wa kunusuru Kaya Masikini Abuodtalib Juma, akichangia katika mkutano huo. 
Ujumbe wa Wawakilishi wa Maendeleo Tanzania wakifuatilia mkutano huowa Wanakaya wa Shehia ya Kikungwi.
Mshauri wa Maendeleo katika Jamii DFID Tanzania Bi Gertude Mapunda Kihunrwa, akitaka kupata ufafanuzi wa mafanikio kwa Wananchi wa shehia hiyo na manufaa gani mamepata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia yao.  
Mwakilishi wa World Bank Bi. Mercy Sabai,akiuliza swali kwa Wanakaya hao kupitia mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini. wakati walipofika katika kaya hiyokujionea maendeleo na mafanikio ya mradi huo kwa Wananchi wa Kaya ya Kikungwi Unguja Wilaya ya Kati.
 Mambo ya fresh madafu hayoo......., Wawakilishi wa Maendeleo wakiburudika na maji ya madatu baada ya mkutano wao na wana kaya. 
                                                            Fresh davu ni tamu sana.
Mmoja wa Mwanakaya anayenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikinin, akiwa nje ya nyumba yake.katika shehia ya kikungwi.  
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF awamu ya Tatu,Ndg. Ladislaus Mwamanga, akiwa katika moja ya nyumba ya Mwananchi wa Kaya masikini katika shehia ya kikungwi, alipofanya ziara kutembelea wananchi wa Kaya hiyo ya Shehia ya Kikungwi akiongozana na Ujumbe wa Wawakilishi wa Maendeleo.   
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladislus Mwamanga, akijificha mvua katika nyumba ya Mwanakaya alioko katika Mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia mradi wa TASAF Awamu ya Tatu uliozinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ndg. Ladislaus Mwamanga akitoka katika nyumba ya Mwanakaya wakati ikinyesha mvua. 
Mwanakaya akiwa na majani ya mgomba akiwapa wageni wake wajifunike mvua, walipofika katika kaya hiyo.

2 comments:

  1. rushwa za chini chini kuwahadaa wazanzibari walewe na fedha ili muungano uendelee , watu bwana wanatafuta kila njia kuwarubuni wazanzibari lakini nasema mara hii hamtupati , labda wanafiki wachache

    ReplyDelete
  2. Acha upumbavu ....wewe umesaidia nini mpaka sasa???

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.