Mshauri muelekezi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Dk. Hamza Hussein Sabri (alie simama) akitoa maelezo na changamoto wanazozipata Kiwandani hapo, kwa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi walipoenda kutembelea Kiwanda hapo.
Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi Hija Hassan Hija akizunguza na uongozi wa Kiwanda cha Sukari na viongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika kuangalia hatua ya uzalishaji Sukari Kiwandani hapo na changamoto wanazokabiliana nazo.
Afisa utumishi wa Kiwanda hicho Bw. Bashir Mohammed akionyesha kiroba cha kilo 50 za Sukari.
Mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Bw. Saleh Suleiman Hamad akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la wawakilishi Sukari iliozalishwa kiwandani hapo ambayo bado haijaingia sokoni hadi sasa.
(Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Kwanza hatuna budi kuipongeza serikali kwa kukifufua kiwanda kihi kupitia hawa wawekezaji. Hii inato picha tosha kwamba kama tukikusudia basi tunaweza kabisa kuwa na viwanda vingi tutavyosaidia kuinua pato la nchi, kuongeza ajira bali kupata unafuu wa bei kwa wananchi wanyonge kwa bidhaa hizi muhimu kwa maisha ya kila siku.
ReplyDeleteWito wangu kwa wawekezaji ni kuwa karibu na wananchi wa maeneo hayo ya Mahonda na maeneo ya karibu ili kuepuka hujma mbalimbali zinazotokea kila wakati. Wasiwatenge wananchi wa maeneo hayo kwa mfano kuwapa ajira zinazostahiki kwa mujibu wa uwezo na elimu zao, sio kila ajira apewe mtu wa nje ya hapo au nje ya Zanzibar kama ilivyo katika sekta ya utaalii.
Serikali ihakikishe hiki kiwanda kinakuwa mkombozi kwa wananchi wanyonge kwa kupata bidhaa hii kwa bei nafuu kabisa, vyenginevyo, hizo subotage zitakuwa haziishi.
Serikali ijitahidi kufanya utaraitbu wa kujitosheleza kwa mazo mengine ya chakula kama mchele na ikibidi ngano kama inakubali kuota a katika ardhi yetu.
Kwa kufanya hivi itaondoa ile dhana ya eti wazanizbari bila ya muungano hatujiwezi kiuchumi!!??
Umeongea kitu chaana sana hasa ulipogusia suala la Corporate social responsibility!
Deletekwakuogezea pia naiomba Serikali itoze kodi nafuu kwa muwekezaji ili aweze kushindana kisoko kwa wale ma -importers.
Rai kwa Company, wanatakiwa waangalie package yao kwa kuweka kiwango tofauti ili mteja mwenye kipato cha chini aweze nunuwa ,kwamfano iwepo japo paket ya 1.5 kg ambayo mzanzibar wa kawaida ataweza kujinunulia.
Ngano??? no wheat along the coast! forget it.
ReplyDeleteAnonymous 4.
DeleteYou may be right that "no wheat along the coast". Lakini nafikiri ni suala la scientific research kuhusu kilimo. Mfano tulikuwa na mawazo kwamba mpunga ni lazima upandwe mabondeni kwenye maji ya kutosha. Nimeshuhudia kwa macho yangu katika kijiji kimoja huko Zanzibar kinaitwa Chutama karibu na Mkwajuni mpunga umestawi maeneo ya juu na ardhi ya mchanganyiko wa udongo na mawe. Nafikiri ni ile mbegu inayoitwa Nerika kama sikosei, kwa hivyo ni suala la tafiti pia linahitajika. mambo mengi ambayo zamani tulidhani hayawezekani katika mazingira fulani leo tafiti zime-prove tofauti.
Mdau wa kwanza kweli umezungumza point ya maana kwani nakumbuka siku za mwanzo baada ya wawekezaji hawa wa Kihindi kupewa hili eneo kulikuwa na hali kutoelewana baina yao na wakulima wa maeneo ya hapo Mahonda, ule mzozo sijui uliishiaje. Lakini kama ulivyosema mwekezaji anapaswa kuwa pamoja na wananchi wa vijiji jirani na kiwanda katika hali mbalimbali, bali hata ikibidi kusaidia kuchangia katika maendeleo ya miradi midogo midogo ya vijiji hivyo. Hii itaondosha kabisa ile risk ya hujma kutoka kwa wanakijiji na watu wengine wa mbali.
Delete