Na
Judith Mpalanzi, Kilombero
SHAMBA
lililokuwa likimilikiwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT)
hayati Daudi Balali, ni miongoni mwa mashamba yaliyofutiwa umiliki na
kukaribisha wawekezaji wapya.
Hayo
yamo kwenye taarifa ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Daudi
Ligazio.
Alisema
tayari mchakato wa kufutwa na kubadilishwa matumizi mashamba hayo zipo katika
hatua za kati.
Alisema
kwa mujibu wa kumbukumbu za halamashauri, wawekezaji wengi hawapo wilayani na
wengine nchini badala yake wamekuwa wakiyatumia maeneo hayo kama
nguzo ya uchumi wao.
“Uamuzi
wa kukufikia hapa ni baada ya halmashauri kubaini kuwa mashamba mengi makubwa
yaliyomilikishwa wawekezaji wilayani humo ni chanzo kikuu cha cha migogoro ya
ardhi kutokana na kutelekezwa na kubaki mapori," alisema.
Alisema
tayari watendaji na wenyeviti wa vijiji wilayani humo wameagizwa kuainisha
mashamba hayo ili zoezi likamilike kwa wakati.
No comments:
Post a Comment