Na Mwandishi wetu
MTU mmoja ameuawa kwa kuchinjwa shingoni na kukatwa
mguu baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe.
Tukio hilo
limetokea katika kijiji cha Tunduni wilaya ya kati Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, marehemu alikutwa na
mauaji hayo baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe mwishoni mwa wiki iliyopita.
Marehemu alivamiwa na watu wenye hasira usiku
akijiandaa kupakia nyama kwenye gari lake
ambayo inaaminika
ilitokana na ng’ombe wa wizi.
Baadhi ya mashuhuda walisema, watuhumiwa wengine wa
tukio hilo
walipigwa na kujeruhiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment