Habari za Punde

Watu 28 wajeruhiwa na mbwa

Na Jumbe Ismailly, IKUNGI
WAKAZI 28 wa kata nne zilizopo tarafa aya Ikungi, mkoani Singida wamejeruhiwa vibaya baada ya kung’atwa na mbwa wanaodhaniwa kuwa na kichaa.

Kata zilizoathirika na tukio hilo lililotokea Februari 22 na Aprili 22, mwaka huu ni pamoja na Mang’onyi, Unyahati, Ikungi, Isuna  kijiji cha Mpetu.

Ofisa afya wa kata ya Ikungi, Agnesi Lucas John, alisema kati ya watu walioumwa na mbwa hao na kufikishwa kituo cha afya cha tarafa ya Ikungi,k 10 ni kutoka kata ya Mang’onyi, Unyahati watu sita,Ikungi watu watano, Dung’unyi  mtu mmoja, Isuna mmoja na Mpetu mmoja.

Alitoa wito kwa watu wanaofuga mbwa wawapeleke mbwa wao kupatiwa chanjo zinazotolewa na maofisa mifugo kwenye maeneo yao.


Aidha, aliagiza mbwa wanaofugwa wafungwe wakati wa mchana ili wasizurure ovyo kwani endapo wazurura wanaweza kukutana na mbwa mwenye kichaa na kushambuliwa na hatimaye nao kupata kichaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.