Habari za Punde

Mkutano wa Ukawa na Waandishi wa Habari Zanzibar.

Naibu Mkurugenzi wa Habari -CUF Taifa Ndg.Abdul Kambaya akionesha barua waliopewa na jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kwa mkutano wao uliokuwa ufanyike leo jumatano na kuahirisha hadi tarehe 30-4-2014, mkutano huo na waandishi umefanyika katika Ofisi za CUF Vuga.   
Naibu Mkurugenzi wa Habari -CUF Taifa Ndg.Abdul Kambaya, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na kuahirishwa kwa mkutano wao na kufanyika mwishoni mwa mwezi huo na kufanyika katika viwanja vya kibandamaiti.na kusema wameridhika na kauli iliotolewa na Jeshi la Polisi Zanzibar kuhusiana na sherehe za Muungano kutimia miaka 50.
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Ndg. Hamad Yussuf, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali  vilioko Zanzibar, uliofanyika katika Afisi za CUF Vuga.
Waandishi wa Habari wakiwasikiliza Viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusiana na mkutano wa Ukawa uliofanyika katika Ofisi za CUF Vuga.

Katibu Mkuu wa BAVICHA Ndg. Deogratias Munishi akizungumza katika Mkutano huo na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano wa Ukawa katika viwanja vya Kibandamaiti. 
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF,akizungumza katika mkutano huo na kutowa maelezo ya matayarishi ya Mkutano huo wa Ukawa unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya kibandamaiti wiki ijayo 30-4-2014. 
Waandishi wakifuatilia mkutano huo wa Viongozi wa Ukawa wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi yaCUF Vuga Zanzibar.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.