Haji
Nassor na Bakari Mussa, Pemba
MAMIA
ya wananchi wa shehia za Wawi,Wara na wapita njia nyengine, jana wameshuhudia
mwili wa marehemu
MOHAMMED
Soud Makame (17), ambae ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika skuli ya
sekondari Vikunguni, amekutwa amekufa
ndani ya nyumba iliyokuwa haijahamiwa katika mtaa wa Wawi wilaya ya Chake Chake Pemba .
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, taatifa za tukio hilo zilitolewa na mtoto
mmoja ambae aliukuta mwili huo ndani ya nyumba hiyo, wakati yeye alipokuwa
akifukuza kuku.
Walisema
baada ya kuuta mwili huo, waliamua kutoa taarifa kwa vyombo husika ikiwa ni
pamoja na polisi, hospitali, sheha wa shehia ya Wawi na baadhi yao
kupiga simu kwa waandishi wa habari juu tukio hilo .
Walisema
waalimkuta marehemu akiwa na kitambaa ambacho wakati wa uhai wake alikuwa
akikivaa kichwani, ingawa kwa jana walikikuta kikiwa shingoni mwake, mithili ya
mtu aliejitia kitanzi.
Sheha
wa shehia ya Wawi, Rashid Issa Juma, alisema alipokea
taarifa za tukio hilo jana majira ya 5:40 mchana, baada baadhi ya wananchi
kuushuhudia mwili huo wa marehemu na ndipo alipotoa taarifa kituo cha polisi
wilaya ya Chake Chake, ambapo baadae walifika kwa shughuli zao za kisheria.
Baba
mzazi wa marehemu huyo, Soud Makame, alisema mwanawe amekuwa na kawaida kila
siku kulala ndani lakini siku ya tukio hakulala, ingawa hakuwa na wasiwasi
wowote kwa vile anaweza kulala hata kwa rafiki wake.
“Kawaida
yake hasa ni kulala nyumbani mwangu, ila juzi ndio hakuja lakini hata mimi
sikuwa na wasisi na leo (jana) nimepokea taarifa ya mshituko kwamba amekutwa
amefariki,” alisema.
Daktari
Ali Hamran Mohamed wa hospitali ya Chake Chake, alieufanyia uchunguuzi mwili wa
marehemu,alisema inaonesha kifo chake kilisababishwa na kuekewa kitu kizito
shingoni.
“Inaonekana
marehemu ama amewekewa kitu kizito shingoni mwake, maana kabla ya kupoteza uhai
ulimi wake umetoka nje, na hasa kwa vile amekutikana na michubuko shingoni,”
alisema.
Hili
ni tukio la nne kwa mwaka huu mkoa wa kusini Pemba
kwa wananchi kuokota miili ya watu waliofariki.
No comments:
Post a Comment