Na
Khamis Amani
KAMPUNI
ya uuzaji wa kuku ya PERDUE iliopo nchini, imo mbioni kukamilisha kiwanda cha
uboreshaji kuku wa viungo na kuuzwa nje ya nchi.
Mara
baada ya kiwanda hicho kukamilika kitawanufaisha baadhi ya wafugaji wa kuku kwa
kuwa na soko la uhakika la kuuzia kuku wao.
Kampuni
hiyo inayouza kuku kutoka nje ya nchi kwa takriban miaka miwili sasa, imesema
hali hiyo itainua kipato cha wafugaji na kuwakwamua katika hali ngumu ya
umasikini inayowakabili.
Hayo
yalielezwa na Meneja Operesheni wa kampuni hiyo, Christopher Kontonasios,
wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema,
kiwanda hicho ambacho kazi yake kubwa itakuwa ni kuboresha kuku waliotiwa
viungo vinavyopatikana Zanzibar na kuuzwa ndani
na nje ya nchi huku wakiwa na utambulisho wa kutengenezwa Zanzibar .
Alisema
kuwepo kwa kiwanda hicho kutapanua ajira kwa vijana, kuwanufaisha wafugaji wa
kuku kwa kukunua kuku wao baada ya kuidhinishwa ubora wao na bodi ya kampuni
hiyo, pamoja na kuitangaza Zanzibar
katika soko la Afrika Mashariki na soko la kimataifa.
Alisema
jengo hilo liliopo Maruhubi linakaribia kukamilik, na wakati wowote kuanzia
sasa vifaa vya awali vitakavyotumika katika kiwanda hicho vitawasili.
Aliiomba
serikali kuwa karibu na wawekezaji na kuwapatia ufumbuzi wa haraka pale
wanapotaka huduma kwa ajili ya vitega uchumi vyao, ili viweze kukamilika katika
wakati uliopangwa.
Kuhusu
bidhaa ya kuku hao, wanaouzwa hapa nchini,
Meneja huyo alisema kuku hao ni
halali na salama kwa mlaji na ni moja ya kuku bora duniani ambao wamepatiwa
vyeti kadhaa vya kimataifa kwa ubora wake.
No comments:
Post a Comment