Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu
cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi
Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika
kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili
huo unatarajia kusafirishwa kuelekea Malawi kwa maziko.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za
mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa
Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita,
wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji baadhi ya
wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi
Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika
kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya
viongozi wa Serikali ya Tanzania na Malawi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa
marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania
Sehemu ya waombolezaji
waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa salamu za rambirambi, wakati wa
shughuli hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa heshima za mwisho mbele ya
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa
shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014
Mabalozi wa Nchi mbalimbali wanaowakilisha Nchi zao Tanzania wakihudguria katika hafla ya kuuwaga mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014(Picha na OMR)
No comments:
Post a Comment