Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza
na Meneja wa Kampuni ya Kimataifa ya uwekezaji vitega uchumi wa Kampuni
ya Lucky Exports kutoka Nchini India Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akisalimiana na Menaja wa Kampuni
ya Lucky Exports ya India
inayoptaka kuwekeza katika sekta za Afya na Viwanda vidogo vidogo vyua mazao ya
Baharini.
Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa
Kampuni ya Lucky Exports Tawi la Tanzania Bwana Kim Mghaya.Kati kati yao ni Meneja wa Kampuni hiyo yenye makao
makuu yake Nchini India Bwana Ravi Rai.Picha na Hassan Issa wa – OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo na ujumbe wa
Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi vya sekta za Afya, Kilimo, Umeme, viwanda
vidogo vya mazao ya Baharini ya Lucky Exports kutoka Nchini India .
Kampuni hiyo ambayo imefungua Matawi yake
katika mataifa mbali mbali Barani Afrika tayari imeshapata usajili wa kufungua
Tawi lake Nchini Tanzania.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini
kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar
Meneja wa Kampuni hiyo Bwana Ravi Rai alisema Taasisi yake imelenga kutoa
huduma za afya pamoja na viwanda vidogo vidogo vya mazao ya Baharini.
Bwana Ravi Rai alisema wakati Uongozi wa
Taasisi yake ukisubiri kuanza na hatimae kukamilisha taratibu zote za uwekezaji
uwekaji wa miradi hiyo umekusudia kusaidia kutoa ajira kubwa kwa wazalendo
pamoja na kuongeza mapato ya Taifa.
Alifahamisha kwamba utafiti wa wataalamu
wa Taasisi hiyo utafanywa ili kuangalia miradi ambayo kampuni hiyo inaweza
kuiwekeza hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
“ Tunafarajika kuona kwamba miradi yoyote
tutakayoamuwa kuitekeleza kwenye uwekezaji wa mataifa mbali mbali duniani
na hasa tukilenga zaidi Bara la Afrika inafadhiliwa na Serikali ya India
“. Alisema Meneja huyo wa Lucky Exports.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema miradi iliyofikiriwa kuanzishwa na
Uongozi wa Kampuni hiyo hapa Zanzibar ya Sekta ya Afya na Viwanda Vidogo
vidogo vya mazao ya Baharini itasaidia kustawisha maisha naustawi wa
Jamii Nchini.
Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Kampuni
hiyo ya Lucky Exports kutoka Nchini India
kurahisisha maombi yao
ya uwekezaji ili taasisi zinazohusika na uwekezaji ziweze kuyapitia na kutoa
maamuzi yanayostahiki kwa wakati muwafaka.
Kampuni ya Uwekezaji ya Lucky Exports ya
Nchini India ambayo tayari
imeshafungua matawi yake katika Mataifa ya Ethiopia ,
Guinea Bisau ,
Malawi na Tanzania inajihusisha zaidi na
uwekezaji wa miradi ya Afya, Kilimo, Viwanda vya mazao ya Baharini, Umeme
pamoja na huduma za Reli.
No comments:
Post a Comment