Na
Haji Nassor, Pemba
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, ameiagiza kampuni ya MECCO
inayojenga barabara ya Wete-Gando na Wete-Konde, kufanya kila juhudi
kuhakikisha kazi hiyo ilioanza tena, haisiti hadi pale watakapoikabidhi
barabara hizo kwa serikali.
Alisema
wananchi wanaotumia barabara hizo wameshachoshwa na ahadi zisizotekelezwa, hivyo
ni vyema kwa sasa wakafanya kila njia kuhakikisha wanazimalizia kwa kiwango cha
lami.
Alitoa
agizo hilo siku
chache baada ya kampuni hiyo kuingiziwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa
ajili ya kuendeleza ujenzi wa barabara hizo.
Alisema
kwa sasa hakuna sababu tena kwa kampuni hiyo kuingia mitini, kwa vile serikali
kwa kushirikiana na washirika wake wa maendeleo ukiwemi mfuko wa Sudia Fund,
kutoa fedha.
Alisema
wananchi wa maeneo hayo wanachotaka sasa ni kutumia barabara hizo katika hali
ya usalama kwa vipindi vyote, sambamba na kuimarisha harakati zao za uchumi.
“Mimi
niinasihi kampuni ya MECCO wajitahidi sana kujenga barabara hiyo kwa mwendo wa
kasi, ili wananchi waanze kuzitumia barabara zao,” alisema.
Akizungumzia
hilo Ofisi Mdhamini wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Ahmed
Baucha, alikiri kwamba kampuni ya MECCO imeanza kazi tena ya ujenzi wa barabara
hizo, ambapo kwa sasa wameanzia na barabara ya Wete-Gando.
Kwa
mara ya kwanza barabara hizo zilianza kujengwa mwaka 2009 lakini ujenzi
ulisitishwa kutokana na serikali na washirika wake wa maendeleo (AfDB) na Mfuko
wa Sudia, kutoingiza fedha kwa wakati.
No comments:
Post a Comment