BUNGE
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana linaanza kikao chake cha bajeti ambapo
muda wa kuchangia na kuwasilisha bajeti za Wizara mbalimbali ukiwa umepunguzwa.
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa shughuli za bunge, John
Joel, alisema, muda wa kuchangia bajeti hiyo umepunguzwa kutoka dakika 10 hadi
saba na muda wa uwasilishaji wa bajeti za Wizara ukiwa umepunguzwa.
Alisema
kutokana na mabadiliko hayo sasa kila wizara itapewa siku moja ya kuwasilisha
bajeti yake na kujadiliwa.
“Tumepima
muda tukaona unatosha,” alisema.
Aidha
alisema bunge litaanza kujadili hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu leo
jioni (jana) kuanzia saa kumi.
Alisema
bunge hilo pia
limeongeza siku za kufanya kazi na litakaa mpaka siku za Jumamosi lengo likiwa
ni kuokoa muda uliopotea.
“Vikao
vitaanza saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana na kutakuwa na mapumziko ambapo
vitaanza tena saa 10 hadi saa mbili usiku na kwa siku za Ijumaa vikao vitaanza
saa tatu hadi saa saba na Jumamosi vitaanza saa tatu mpaka saa saba,” alisema.
Alisema,
bunge hilo
litaendelea hadi tarehe Juni 27.
Pia
alisema kwa mujibu wa ratiba bajeti inaweza kusomwa Juni 12, mwaka huu.
Katika
kikao cha jana, wabunge wawili wapya Ridhiwani Kikwete na Godfyey Mgimwa,
waliapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa wabunge.
No comments:
Post a Comment