Habari za Punde

Mkutano wa hadhara wa CCM Ulioandaliwa na Wajumbe wa Barazala Wawakilishi wa CCM Nungwi.

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Kupitia UWT Mh. Asha Bakari Makame akimwaga sera wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Nungwi na kuandaliwa na Wawakilishi wa CCM Zanzibar.
Kijana Mashu Kombo aliyetoka Chama cha Upinzani cha CUF na kurejea Chama cha Mapinduzi  akielezea msimamo wake uliopelekea kurejea chama hicho huku akishangiriwa na Kijana wa Kimasai kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja.
Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mh. Salim Awadh Salmin akielezea msimamo wa kamati yake wa kupeleka hoja binafsi Barazani  wakati ukifika ya kuulizwa Wananchi wa Zanzibar kama bado wanaendelea kuridhika na mfumo uliopo  wa  uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Kupitia UWT Mh. Asha Bakari Makame akimwaga sera wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Nungwi na kuandaliwa na Wawakilishi wa CCM Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akikabidhi seti za Jezi na mipira kwa Vilabu 18 vya soka vya Jimbo la Nungwi vilivyotolewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CCM kuimarisha mchezo wa soka ndani ya jimbo hilo.Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji juma Haji.Mmoja wa Vijana wa CCM waliohudhuria mkutano wa Hadhara wa Chama hicho ulioandaliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wa CCM akionyesha furaha yake kutokana na sera zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa chama chake.

Baadhi ya Wanachama wa CCM Jimbo la Nungwi wakionyesha ishara ya kuunga mkono msimamo wa chama chao wa kuendelea kutetea mfumo wa serikali Mbili katiba mfumo wa katiba mpya ya Tanzania.
Vijana wa Kikundi cha utamaduni cha ngoma ya Mchikicho Kutoka Nungwi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika jimbo lao baada ya Kikundi hicho kutoa burdani safi katika mkutano huo.

1 comment:

  1. Msipoteshe hao maskiin wa Allah! Hawajuwi kitu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.