Habari za Punde

Mnada wa samaki Bandari ya Msuka, Pemba

 
WACHUUZI wa samaki katika bandari ya Msuka, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa wamezunguka mnada wa samaki bandarini hapo, kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.

SUALA la mabadiliko ya Tabia nchi, limekuwa likiathiri sehemu mbali mbali ksiwani Pemba, pichani ni mashina ya miti ya mikoko iliyoliwa na maji ya bahari, huko katika bandari ya Msuka Wilaya ya Micheweni Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

2 comments:

  1. Utaratibu huu wa kufanya biashara katika mazingira yasiyoeleweka sasa umeshakuwa ni utamaduni wetu. Inashangaza sana wazanzibari tuna uzoefu wa biashara kwa zaidi ya miaka 500, lakini biashara zetu nyingi ziko shaghala baghala kweli. Ukienda pale bandari ya Nungwi kuna soko zuri sana, lakini minada ya samaki inafanyika chini ya mkungu chin kabisa kwenye mchanga!!, Ukienda Darajani hapa ndio aibu kabisaaaaaaaaa! minada nje ya soko juu ya mafuniko ya makaro, chini kabisaaa, ukienda Malindi kuna soko zuri kabisa, watu wanauza samaki nje ya soko some time chini kabisaa, sijui tuna nini sisi wazanzibari, la kushangaza kama vile hii hali tumeshaikubali kuwa ni sehemu ya utamaduni wetu, kwa sababu wengi wetu tumesoma na tumeelimika na tunajua vyema suala la hygiene lakini sijui ni mapuuza au kuwa care free!!
    Tubadilikeni jamani, utamaduni huu wa kufanya biashara katika mazingira machafu si ustaarabu jamani.

    ReplyDelete
  2. Hiyo mikoko haikuliwa na bahari bali imekatwa na binaadam - baadae binaadam hao hao hulalama kuwa maji ya bahari yanaingia kwenye mashamba yao na maeneo wanaoishi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.