Habari za Punde

Stendi kuu ya Daladala Chakechake



KUFUATIA kuongezeka ka maduka ndani ya soko kuu la Chake Chake, limepelekea kuifanya steni ya dalala kuwa ndogo na kupelekea usumbufu wa magari mbali ya abiria kuingia na kutoka, kama inavyonekana katika picha.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

1 comment:

  1. Yale yale kama ilivyo Unguja naona na Pemba nako yanakuja. No town planning. Kwani wenye kutoa ruhusa ya kufanya biashara ni nani? na wenye kumiliki eneo la Stand ya magari ni nani?? Ni taasisi moja, sasa wanachokifanya ni nini, au wanajali mapato tuu bila kuangalia consequences, kwa mtazamo si muda mrefu hilo eneo lote litakuwa ni sehemu ya maduka!! na wenye magari wataondoshwa, itakuwa kama Unguja vituo vya daladala vipo njiani, ajabu, Only in Zanzibar!!

    Halaafu mimi nina wazo moja. Hizi gari aina ya "Chai magarage", kwa kweli hasa zimepitwa na wakati tena jamani, si hivyo tu bali hasa ni maudhi hasa kupanda na zikiwa zimejaa. Binafsi, nikienda Pemba basi moja ya gamu niliyonayo ni hiyo, utakuta gari imejaa watu kabisa, mizigo humohumo, wenye kuku wao, wenye bidhaa zao humohumo, hee huwa taabu kwa kweli.
    Ushauri wangu hasa kwa wafanyabiashara ambao Allah amewajaalia neema ya kipato kidogo, wajaribu kufanya mabadiliko/mapinduzi katika sekta ya usafirishaji wa abiria na mizigo, mfano kuleta magari (mabasi) yatayokuwa na nafasi zaidikwa abiria na mizigo. Tubadilike kidogo na hili linawezekana wala sio gumu sana. Ni suala la wenye nafasi(uwezo) kujali na kulitilia maanani. Pemba itapendeza kweli, Inahitaji watu ku-sucrifice kwa ajili ya Kisiwa chetu, kama tunavyoona sasa hali miji hasa wa Chake inavyobadilika kwa majengo ya ghorofa ya kupendeza.
    Inawezekana tujenge kisiwa chetu. Pemba na Zanzibar kwa ujumla.

    Wassalaam

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.