Habari za Punde

Picha na matukio kutoka Pemba

 MWALIMU mkuu wa skuli ya sekondari ya Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Hamad, akiwaonyesha wajumbe wa Jumuia ya watu wa Kengeja ‘KEDO’ waishio Dar –es Salaam, msingi wa jengo la madarsa , mara baada ya ujumbe huo kukabidhi vifaa kadhaa kwa skuli hiyo (picha na Haji Nassor, Pemba)


 WAISLAMU wa kijiji cha Kambini kichokochwe wilaya ya wete Pemba, wakiwa katika kazi za usafi wa kung’oa majani kwenye jengo lao jipya la msikiti, mbalo wanalijenga kwa nguvu zao, huku msaada ukihitajika ili wahamie (picha na Haji Nassor, Pemba)
KATIBU wa Jumuia ya Mazingira ya shehia ya Kambini Kichokochwe ‘JUMAKA’ wilaya ya wete Pemba, nd:  Bakar Suleiman Juma, akigagua kitalu chao cha miche 5,000 ya mikarafuu, ambapo wiki ijayo wanatarajiwa kuwauzia wananchi na serikali (picha na Haji Nassor, 


HALI ya majengo ya afisi za askari wa magereza eneo la Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, imekuwa ya kusikitisha kutokana na kuchakaa kwa muda mrefu, na kuwapa hofu askari hao, ambapo kwenye jengo hili wakizungumza na watendaji wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)



2 comments:

  1. CCM Oyeee!!!!
    Muungano wa Miaka 50 Oyeee!!!
    Serikali mbili Oyeeee!!!!

    Kituo hicho nafikiri ni kama kile cha Unguja Kunua Miguu. ambacho kilijengwa na Wakoloni .. Serikali ya SMZ licha yakujigamba kwamba Muungano unafaida, inauma ikiwa hawazioni hizi ni moja ya Changamoto ya kuwa na Serikali 2 za Muungano.

    Nikisema hivo najua Magereza haiko kwenye Muungano, lakini kutokana na Kero za muungano na Zanzibar kushindwa kuamua hatma ya mambo yake ya maendeleo ndio yanapelekea matatizo ya jamii kama haya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous 1
      Mimi nakubaliana nawe kwamba Muungano huu usio na utaratibu wa kueleweka inaweza kuwa moja ya sababu ya hapa tulipo na hayo yanayoitwa maendeleo. Lakini pia nafikiri kwamba uendeshaji wa taasisi nyingi za SMZ una mashaka sana hasa kwenye hizi taasisi za kiaskari. Nitakupa mfano, hao magereza wana vitega uchumi vingi sana hasa hapa Unguja, lakini ni dhahiri mapato yote yanaishia kwa watu wachache, na hivyo kushindwa kuendeleza hata majengo yake.
      Mwaka 1993/94 tukiwa JKU kwa mujibu wa sheria mara baada ya kumaliza form six, tulipelekwa Bambi, tulitarajiwa kukaa kwa mwaka mmoja. Cha kushangaza kabla ya kumaliza mwezi tulianza kurudishwa mjini eti sababu ni kukosekana kwa chakula hapo kambini??!! La ajabu sisi wenyewe tulikuwa tukifanyishwa kazi kwenye mashamba binafsi ya Maafande (mashamba ya viazi n.k) na tukivuna kwa wingi sana.
      Kwa hiyo utaona kuwa hivi vikosi vya askari vya SMZ ni chaka la walaji kwa wakubwa.
      Vipo hapo kuwanufaisha wakubwa tuu.

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.