Habari za Punde

Ukawa katika Picha walipokuwa Pemba

 KATIBU Mkuu wa CUF na makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Mhe: Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia wananchi mbali mbali na wafuasi wa vyama vya CUF, DP, NCCR- MAGEUZI, kwenye mkuatano maalum wa ushirikiano, uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
 
WAANDISHI wa habari wa vyombo mbali mbali, wakiwa kazini kwenye mkutano uliohusisha wafuasi wa vyama vya CUF, NCCR-MAGEUZI, na DP ambao umefanyika kwa vyama hivyo kuunga nguvu ya pamoja ilionzia kwenye bunge la katiba (picha na Haji Nassor, Pemba)

 
Katibu Mkuu wa chama cha siasa cha CHADEMA taifa Willbroad Slaa, akiwa pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA akizungumza na wananchi na wafuasi wa vyama kadhaa vya siasa, kwenye uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)


 
 
WAJUMBE waliokuwa wa bunge maalum la katiba ambao waliotoka nje ya bunge hivi karibuni, wakiwasalimia wananchi wa Pemba, kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,  mkutano huo ulifanyika uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)


WAFUASI wa vyama vya CUF, CHADEMA na DP wakinyoosha mikono yao juu kuashiria kuunga mkono kwa vyama hivyo kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi mkuu ujao, hayo yajiri kwenye mkutano wa pamoja wa vyama hivyo uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)




MWENYEKITI mwenza wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Christopher Mtikila, akizungumza na wananchi na wafuasi wa vyama vya DP, NCCR-MAGEUZI, na CUF mkutano huo maalum uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)

4 comments:

  1. maalim seif ww ni kiongozi mzuri lkn umri ushakuwa mkubwa muandae mtu wakuja kuvaa viatu vyako kwa dalili inaonekana hujamuandaa mtu hiyo ni hatari kwa chama chako watu watakuja kugombana kwa madaraka siku mungu akikuchukua mm naona ungemuandaa mtu wakugombea urais mwakani wa znz halafu ww ukamsimamia huo ni ushauri kama ntawakera kwa coment yangu nisameheni

    ReplyDelete

  2. Ndugu mdau wa pili 4:36pm ni kuwa maalim Seif hivi sasa tayari mtu amekwishamuandaa.Na kwa fununu zilizopo ni kuwa kijana Jussab,machachari na mahiri,ana dam changa na hata kuoa bado na anaziweza purukushani za kimipacho,kwa hivyo toa wasiwasi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous 3.
      Kama hhizo fununu zitakuwa na ukweli basi Kijana Jussa na afanye ''nusra haraka'' kwani kwa post kama hiyo suala la zawaaj pia lina uzito kwa hapa kwetu.

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.