Na Khamisuu Abdallah
JESHI la Polisi Zanzibar, linawashikilia
watu saba kwa tuhuma za kutekeleza
shambulizi la bomu katika maeneo ya Darajani
na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa.
Akizungumza na gazaeti hili ofisini kwake
Ziwani, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa jeshi la polisi,
DCI, Yussuf Ilembo ,alisema watuhumiwa hao walikamatwa
Juni 18 mwaka huu majira ya usiku katika maeneo mbali mbali ya mi wa Zanzibar .
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya
watuhumiwa hao akisema bado upelelezi unaendelea.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu
ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Aliwataka wananchi kuacha kufuata
vishwawishi na kurubuniwa na watu au makundi ya kihalifu kwa lengo la kuchafua
amani na kuwatia hofu wananchi.
Tukio hilo la bomu lilitokea wika Juni 13 majira ya
saa 2:30 za usiku katika maeneo ya Darajani ya mjini Unguja na kuwalenga
wahubiri wa amani wa dini ya kiislamu waliokuwa nje ya msikiti.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Kassim Issa
Muhammed (36) ,Hamad Nassor Kassim (46) , Khelef Abdalla Abdalla (21), Khalid
Ahmed Haidar (16) , Ahmed Haidar Jabir (47) na
Suleiman Ali Juma (21) huku marehemu akitambulika kwa jina la Mohammed
Khatib Mkombalaguha (26) mwenyeji wa Tanga.
No comments:
Post a Comment