Na
Masanja Mabula,Pemba
SERIKALI
ya mkoa wa kaskazini Pemba, imeelezea kusikitishwa na uchakavu wa makaro katika
nyumba za maendeleo Mtemani wilaya ya Wete na kuagiza taasisi husika kuyafukia
ili kuepusha uwezekano wa kutokea maradhi ya mripuko.
Mkuu wa
Mkoa huo, Dadi Faki Dadi, alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watendaji wa
Wizara ya Majenzi, Baraza la mji Wete,Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na
Shirika la Umeme Pemba.
Alisema
ni vyema taasisi hizo kushirikiana pamoja na kuyafukia makaro hayo ambayo
yamekuwa yakitiririsha maji machafu yenye vinyesi vya binadamu.
"Hili
ni tatizo na linatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka ili kunusuru afya za wakaazi wa nyumba hizi kupata maradhi ya
mripuko,”alisema.
Katika
hatua nyingine Dadi aliagiza migomba iliyopo bloke namba nne na tano yang’olewe
ili kudumisha hali ya usafi.
Akizungumza
kwenye kikao hicho, Ofisa Mdhamini
Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Pemba, Hemed Salim, alisema tatizo la nyumba
hizo linakwamishwa na ufinyu wa bajeti.
Alisema
tayari wizara imeomba fedha kwa ajili ya matengenezo ya nyumba hizo na kwamba
wanatarajia kupatiwa fedha hizo kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
"Tatizo
lipo na linasababishwa na ufinyu wa bajeti, lakini tunatarajia kwamba hali hiyo
itaondoka katika kipindi hichi cha fedha kwani tumeomba fedha kwa ajili ya
matengenezo ya nyumba hizi,” alisema.
Serikali jengeni mji mwengine wa kisasa. Musikae hapo mpaka Leo kubwabwaja maendeleo ya mzew Karume. Nyie mumefanya lipi kubwa. Jengeni new town unguja na pemba.
ReplyDelete