Na Kadama Malunde,Shinyanga
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda, amewataka
viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na serikali na kuliombea taifa kutokana na kuanza kuibuka
matukio ya ugaidi ambayo yanatishia amani iliyopo.
Akizungumza kwa niaba ya Pinda, Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Rais,Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira, alisema viongozi wa
dini hawanabudi kuunganisha nguvu kwa pamoja kulaani vikali vitendo hivyo viovu
,kwani ni hatari kwa taifa.
Alikuwa akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la parokia ya
Usanda ya Papa John Paul wa II lililopo Tinde mkoani Shinyanga.
Aidha
alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na taasisi za dini kuwekeza kwenye elimu,afya na huduma nyingine
muhimu katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Awali katika ibada iliyoongozwa na Makamu wa Askofu jimbo
Katoliki la Shinyanga,Padri Sospeter Sholle,alisema kuporomoka kwa maadili
katika jamii ni mambo yanayochangia kupata viongozi wasiowaadilifu, wabinafsi
na waroho wa madaraka.
Akiwasilisha ujumbe uliotolewa na baraza la maaskofu Tanzania
kuhusu katiba mpya, Padri Shole, alisema bunge maalumu la katiba linatakiwa
kuzingatia maoni ya rasmu ya pili ya katiba,kwani Watanzania wanahitaji kuwa na
katiba itakayojali utu wa kila mmoja,kuzuia matumizi mabaya ya madaraka na
ufisadi.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa hilo
ambalo litaitwa Papa John Paul wa II, Padri Dk. Emmanuel Makolo, alisema ujenzi wake mpaka kukamilika
unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi
milioni 244 na kuwaomba Watanzania na wadau mbalimbali kuchangia ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Mgeni rasmi katika harambe hiyo angia
shilingi milioni 6.
No comments:
Post a Comment