Wizara ya Elimu yachukua hatua
Uchunguzi
wabaini ukweli wa madai hayo
Na
Khamisuu Abdalla
SIKU
mbili tu baada ya gazeti hili kuchapisha habari kuhusu wanafunzi kusomeshwa
bibilia na kutakiwa kutokwenda skuli wakiwa wamefunga, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali, imefanya uchunguzi na kubaini kwamba tuhuma hizo ni za kweli.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ofisini kwake Majestik, Mrajisi wa Elimu Zanzibar, Siajabu
Suleiman Pandu, alisema baada ya uchunguzi kufuatia habari, waligundua
malalamiko ya wazazi ya wanafunzi ni ya kweli.
Alisema
alipohojiwa, mmiliki wa skuli hiyo inayoitwa Eden International,Pilsoon Youn
(maarufu mama Kim), alikiri kwamba anatoa elimu ya bibilia kwa wanafunzi.
Alisema
katika kuta za madarasa kumebandikwa vipande vya aya za bibilia ambavyo vinathibitisha kwamba bibilia
inasomeshwa.
Hata
hivyo, alisema bibilia inafundishwa huku idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma
katika skuli hiyo ni Waislamu.
Mrajisi
huyo alisema baada ya kuwahoji wanafunzi walielezea kusikitishwa kutosomeshwa
dini yao (Uislamu) licha ya wingi wao madarasani na badala yake kufundishwa
bibilia.
Aidha
alisema hata mavazi ya wanafunzi hayaridhishi kwa sababu wanafunzi wa kike wa
kiislamu hawaruhusiwi kuvaa hijab.
Alisema
kulazimisha wanafunzi kusoma bibilia ni kinyume na katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984 na Muungano ya mwaka 1977, ambazo zimetoa uhuru kwa mtu kufuata dini
aitakayo bila kulazimishwa.
“Hakuna
kosa mtu kufundisha dini bali ni kosa kuwalazimisha watoto kusoma dini ambayo
sio ya kwao,” alisema.
“Wakati nilipokuwa nikipata maelezo kutoka kwa
baadhi ya wanafunzi wa kiislamu wanaosoma katika skuli hiyo walisikitishwa sana
kutosomeshwa dini yao licha ya kuwa wingi madarasa na badala yake kulazimishwa
kusoma bibilia,” alisema Mrajis huyo.
Alisema
sheria ya elimu kifungu 47 hadi 48 kinasema kuwa skuli au tasisi za kidni
zinaweza kuanzishwa chini ya sheria hiyo
kifungu kidogo (2) pale skuli au tasisi za aina hii zinapoanzishwa masharti ya
kifungu
Kifungu
cha 13 (3) cha sheria ya elimu namba 6 ya mwaka 1982,kinasema skuli au tasisi za kidini hazitojumuisha
darasa au mafundisho mengine ya kidini yanayotolewa misikitini, makanisani au
katika sehemu nyengine zozote za ibada mradi tu darasa au mafundisho hayo ni ya
kidini kwa kila hali.”
Aidha
kifungu cha 48 cha sheria hiyo kinasema: “Bila kujali masharti ya kifungu cha 47 cha sheria
hii (namba 6 ya 1982) mafundisho ya kidini yataweza kutolewa katika skuli
yoyote ya serikali au binafsi au inayosaidiwa, mradi tu wakati wa utekelezaji
wa masharti ya kifungu hiki, imani za kidini mbalimbali walizomo wanafunzi
zitazingatiwa ili kuhakikisha mwanafunzi anapatiwa mafundisho ya dini ile
inayomruhusu.”
Alisema
mmiliki wa skuli hiyo alikuja Zanzibar kama
taasisi ya Africa Agape Assosiation, kwa ajili ya kuanzisha skuli na kusomesha
watu masuala ya kidini na kumjua mungu.
Hata
hivyo, alipofanya kikao na wazazi wa wanafunzi kabla ya kuandikishwa,
aliwahakikishia kwamba skuli hiyo haitafundisha dini ya aina yoyote.
Mrajisi
huyo alisema wizara tayari imeshajipanga kuhakikisha hatua nyengine za kisheria
zinachukuliwa.
“Sisi kama Wizara tayari tumeshajipanga na
tunaendelea kujipanga kulifanyia kazi suala hili kwa kuliandikia ripoti ili
hatua nyengine zichukuliwe kwani kama Mrajisi sina mamlaka ya kuifungia skuli hii bali wenye
mamlaka ni Baraza la Elimu,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu usajili wa skuli hiyo, alisema kwa mujibu wa taarifa aliyoipata Mamlaka
ya Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) usajili wa skuli hiyo sio wa kudumu na kwamba ilisajiliwa kwa namba RPS/329 mwaka
2010/2011.
Lengo
la kutoa usajili wa muda ni kutoa nafasi ya kuchunguza malengo na dhamira yake
kabla ya kupewa usajili wa kudumu.
Alisema
katika kuondoa matatizo kama hayo, wameanzisha msako wa kutafuta skuli ambazo
hazijasajiliwa ambapo tayariu skuli 40 zimekamatwa.
Akizungumzia
madai ya skuli ya Karibu ya Kijichi ya
mwalimu kuwalazimishwa watoto kuweka maji mdomoni katika kipindi hichi cha
Ramadhani, alisema tayari mwalimu aliefanya kitendo hicho ameshafukuzwa skuli.
Hivi
karibuni mama Kim ambae ni raia wa Korea, aliwataka wazazi wa wanafunzi wa
skuli ya Aden kuwahamisha watoto wao kama wanashindwa kutekeleza masharti.
Aidha
alikiri skuli yake kufundisha bibilia na kuwalamisha wanafunzi waliofunga
kutokwenda skuli.
Kauli
ya mama Kim, ilikuja baada ya wazazi wa wanafunzi hao, kusema watoto wao
wanafundishwa bibilia na kulazimishwa kwenda skuli na chakula wakati wamefunga
au kutokwenda skuli kabisa.
Wacha tulipe gharama za ujinga kidogo!
ReplyDeleteHaya ni matokeo ya Taasisi za kiislamu kushindwa kuona mahitaji ya wakati kwa waumini wao kwamba sio misikiti na madrassa peke yake bali skuli pia!
@Adhubany Nakubaliana nawe kwa upande mmoja, mila nashauri tusiwazilaumu hizi Taasisi za Kiislam kwa sasa kwani lawama hazitasaidia. La msingi tukae nazo tuzielimishe na tuzishauri kwamba kuna ulazima sasa kuwa name skuli, hospital bora za kiislam, kwani hata kwenye sekta ya afya nako kuna matatizo hasa kwa mama zetu wakati wa kujifungua maadili ya kiislam yanakiukwa sana
Delete