Na Farida Msengwa, Morogoro
WASHTAKIWA watatu
wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mtoto Nasra Rashid Mvungi, wamebadilishiwa
Hakimu baada ya hakimu wa mwanzo kupata dharura.
Washtakiwa hao ambao
kesi yao imekuwa ikifikishwa na kutajwa mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa
mahakama ya hakimu Morogoro, Mary Moyo, walipandishwa kizimbani mbele ya hakimu
Agripina
Kimanze na kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Kufuatia hali hiyo,
washtakiwa hao walichelewa kupanda kizimbani tofauti na nyakati nyingine, hali
iliyoonekana huenda ilisababishwa na mabadiliko hayo.
Mwendesha Mashtaka
wa Polisi,Aminatha Mazengo, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo
bado haujakamilika na kwamba jalada bado lipo kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali,
hivyo kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Mahakama imeridhia
ombi hilo na kupanga Agosti 20 mwaka huu kufikishwa tena kwa kesi hiyo kwa ajili
ya kutajwa, kutokana na mahakama hiyo kukosa uwezo kisheria kusikiliza shitaka
la mauaji.
Kesi hiyo ya mauaji
inawakabili washtakiwa watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto Nasra,Rashid Mvungi
pamoja na waliokuwa walezi wake, Mariam Said na mumewe Mtonga Omary, ambao
awali walikuwa wakikabiliwa na shtaka la kula njama na kufanya vitendo vya
ukatili dhidi ya marehemu kabla ya shitaka lao kubadilishwa baada ya mtoto huyo
kufariki.
No comments:
Post a Comment