Na Abdi
Suleiman, PEMBA
WANANCHI
kisiwani Pemba, wametakiwa kujenga misingi ya kuwafahamu watu wenye ulemavu na
kujuwa mbinu mbali mbali za kuishi na watu hao.
Wito huo umetolewa na washiriki wa Mkutano wa wadau wa kutoafursa
kwa watu wasioona, uliondaliwa na Jumuiya ya ZANAB Pemba .
Washiriki hao walisema kuwa, kama
jamii ingejenga misingi ya kuwafahamu wenye ulemavu, jinsi gani wanapaswa
kuishi nao pamoja matatizo yote hayo yanayowakumba yasingetokeoa.
Mmoja kati ya washiriki hao, Nassor Hafidh kutoka Jumuiya ya
Maimamu, alisema kuwa walemavu wa akili wamekuwa wakidhalilishwa kutokana na
ulemavu wao.
Alisema kuwa walemavu wasioona wana afadhali katika matukio ya
udhalilishaji kuliko walemavu wa akili, jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo ya watu wenye ulemavu.
“Tatizo la yote hao ni ukosefu wa taaluma kwa jamii, jamii iliyo
kubwa inaonekana haina elimu, jinsi gani waishi na watu wenye ulemavu”alisema.
Yussuf Hamad kutoka kitengo cha askari wa usalama wa barabarani
Mkoani, alisema kuwa Serikali inapaswa kuwashirikisha watu wenye ulemavui kwa
kila kitu, sio kuamua jambo bila ya kuwashirikisha hali inayopelekea kuwepo kwa
usumbufu baadae.
Alifahamisha kuwa, watu wenye ulemavu wanapaswa kuwekwa karibu
katika nafasi mbali mbali za ajira kama ilivyo
watu wasio na ulemavu.
“Ajira nyingi zinatolewa ingewekwa angalau alisimia 15% nao
wanaajiria, lanini hilo
halipo hata ukiangalia majimba
yanayojegwa hayako rafiki nao pia”alisema.
Ramadhan Khamis alisema kuwa, kuwepo kwa sheria ya walemavu Zanzibar ni moja ya taua
moja mbele, hali ambayo ingekuwa ni nafuu kwao.
Aliyomba serikali kuwapatia walemavu wa sio mashine za nukta
nundu, ambayo itaweza kuwasaidia katika masomo yao , kwani walemavu wasioona wamekuwa wakipata
tabu wakati wanapohitaji kusoma.
“Utamuona kiongozi anamiliki gari la Milioni 30, lakini
kumsaidia mlemavu braina moja ni tatizo kubwa kwakwe, tuwaone hawa ni vijana
wetu”alisema.
Kwa upande wake Sabra Nassor kutoka ZANAB Pemba, alisema kuwa
suala la elimu mjumuisho kwa walemavu wasiona ni tatizo kubwa sana kwao.
Sabra alisema kuwa, wanafunzi wenye ulemavu wa kutokuona ip[o
haja ya kuwekwa pamoja katika skuli zenye bodingi, ili kuweza kusaidiana wakati
wa masomo.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo, mratib wa Jumuiya ya watu
wenye ulamavu wa akili Pemba , Ali Haji Mwadini
alisema kuwa, tatizo la kubakwa watu wenye ulemavu bado linaendelea kutendeka
kutokana na ulemavu wao.
Alifahamisha kuwa, laiti kama
wabakaji hao wangekuwa wakitiwa hatiani basi matendo hayo ya kubakwa na
kudhalilisha kwa walemavu lingepungua.
Mratib huyo alisema kuwa, kwa sasa watendaji wa vyombo vya
sheria wanapaswa kukubaliana na ushahidi unaotolewa na walemavu mahakamani pale
wanapofanyiwa udhalilishaji.
Alifahamisha kuwa, sasa wakati umefika kwa serikali kujenga
majengo yatakayofuata suala la mujumuisho wa watu wote, kwani majengo mengi
yamekuwa ni kikwazo kikubwa wa walemavu wasioona na hata wengine.
No comments:
Post a Comment