Sajenti Ali Kassim akitowa mafunzo kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni jinsi ya matumizi ya barabara kwa watumiaji wa kutembelea kwa miguu ili kuepusha ajali wakati wanafunzi wanapotoka Skuli, Mafunzo hayo yameanza kutolewa kwa Wanafunzi wa skuli hiyo na kuendelea kutolewa kwa Wanafunzi wa maskuli yote Zanzibar. Wanafunzi ni wadau wakuu katika matumizi ya barabara wakati wa kutoka skuli na kwenda.Mafunzo haya ya vitendo yametolewa katika barabara ya Darajani jana.
Askari wa Usalama barabara akisimamisha magari wakati wa kutowa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni jana.
Wanafunzi wakikata barabara wakati wa zoezi la mafunzo kwa vitendo lililokuwa likitolewa kwa Wanafunzi hao jana. 
Hivi ndio inayotakiwa,kuna baadhi ya wanafunzi hapo tayari watakuwa ndio warithi wa kazi hiyo ya usalama barabarani miaka ijayo,wanachotakiwa walimu sasa i kujua ni mwanafunzi gani alieipenda kazi hio na kama anataka kazi hio kuwa ndio kazi ya ndoto yake ili aanze kpikwa ili nchi ipate vipaji vya uhakika hapo baadae kwani mfanyakazi anaeanza kuipenda kazi yake kutokea uttoni na kuifanyia kazi hadi kufikia maleng hayo sio sawa na kumuajiri mtoto wa shangazi au mjomba kaa ilivyozoeleka hapo kwetu Zanzibar,
ReplyDeleteTunaomba sio tu kama hao wanafunzi waishie hapo barabarani bali pia wapelekwe mahospitalini waone jinsi kazi za udaktari zinavyoendeshwa na jinsi ya kuhudumia wagonjwa vijana wapewe nafasi hata ya kusaidia kutoa huduma ndogndogo kwa wazazi na watoto wagonjwa mashuka yao au kutoa yoyote ili kuwaangalia na kugundua vipaji vyao ili kuboresha akili za vijana hao ambao wanahitaji kusaidia kama tunataka maendeleo hapo nchini,pia wanafunzi wapelekwa wizara ya habari na waonyeshwa utendaji mzima wa shughuli za pale kama utangazaji,upigaji picha,uchukua wa video,magazeti;mitambo na mambo mengi ya kazi hizo,jingine ishiishie hapo tu wapelekwe kwenye sehemu za wizara ya umeme waonyeshe shughuli zote na utendaji wake,majenzi,bandari,uvuvi,kilimo, na mwisho atatakiwa kila mwalimu atoe ripoti ya wanafunzi hao wadogo ni kazi gazi kati ya hizo amevutiwa nazo ili aanze kuendelezwa kila mmoja na shughuli yake kwa kiwngo cha hali ya juu, Wapelekeni baraza la uwakilishi waangalie utendaji wa kazi za hapo,kuna vijana wana uwezo mukubwa wa ungozi hao ndio wanatakiwa kuendelezwa hapo maskuli na kuanza kuwatumia kama viongozi wa wenzao wengine kuelekea katika uongozi wa ngazi za juu hapo nchini miaka ijayo,
JE MPAKA HILI AJE BWANA MZUNGU HUKO AFRIKA AKUFUNDISHENI?