Na Benedict Liwenga, Maelezo
UMOJA wa Machifu Tanzania
(UMT), umewasilisha nyongeza ya mapendekezo yake kuhusu katiba mpya kwa Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samia Suluhu Hassan.
Akiuwakilisha umoja huo, Chifu kutoka Magu, John Nyanza,
alimueleza Samia kwamba wanaishauri serikali kutayarisha mkakati wa kitaifa wa
utamaduni ili mpango mkakati huo uwe dira ya utamaduni.
Naye Chifu kutoka Ntuzu
Bariadi, Agnes Ndaturu, alisema mapendekezo yao yatasaidia kuwatambua waganga
wa jadi pamoja na mipaka ya kazi zao.
“Mapendekezo haya yatasaidia
viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga wanaokiuka maadili
ya shughuli zao mfano mauaji ya albino, kwa kuwa kila kiongozi atakuwa anawatambua
waganga wa eneo lake,” alisema Chifu Ndaturu.
Alisema wajumbe wenzao
waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya umuhimu wa utamaduni kupewa
nafasi rasmi katika katiba mpya na serikali ili pawepo kipaumbele katika
utekelezaji wake nchini.
Wakizungumza kwa kauli moja,
walisema suala la utamaduni katika rasimu ya pili ya katiba lifanyiwe
marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo yaliyobainishwa huku msisitizo wao ukiwa
katiba kueleza wazi sera na sheria mpya zitakazotungwa zihakikishe Tume ya taifa
ya utamaduni inaanzishwa.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, aliwatotoa wasiwasi wawakilishi wa umoja
huo kwamba atayawasilisha katika Kamati ya Uongozi ya Bunge.
No comments:
Post a Comment