Habari za Punde

SMZ Itaendelea Kuwasaidia, Kuwaendeleza na Kuwawezesha Vijana wa Zanzibar ili Kuweza Kujikwamua Kiuchumi .

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Shaib Ibrahim Muhamed akizungumza na Vijana kutoka Vikundi  mbali mbali huko katika Ukumbi wa Kariakoo,Wilaya ya Mjini.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Shaib Ibrahim Muhamed amesema wataendelea kuwasaidia, kuwaendeleza na kuwawezesha Vijana wa Zanzibar  ili kuweza kujikwamua kiuchumi .

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Kariakoo wakati wa Kikào cha  robo  mwaka cha Uratibu  wa shughuli za Maendeleo ya Vijana Zanzibar.

Amesema  jukumu la Idara hiyo ni kuratibu na kusimamia Vijana kupitia Baraza la Vijana  kwa  kuwapa  muongozo wa kitaifa na kuwapatia taaluma ya kuwajengea uwezo ili kuhakikisha shughuli mbali mbali za maendeleo ya Vijana zinafanyika ipasavyo.

Aidha amewataka Vijana hao kushiriki katika zoezi la kupiga kura  kwa Amani na utulivu ili kuendeleza Uzalendo wa nchi yao.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Ali Haji Hassan amesemà Serikali imeanzisha Mabaraza ya Vijana Kwa lengo la kuimarisha mashirikiano ya Vijana na Wadau Mbali mbali katika ngazi ya Sheria na Wilaya ili kufikia malengo ya kuwainua Vijana .

Kwa Upande wa Muakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Idadi ya Watu ( UNFPA) na Masuala afya ya Uzazi . Amina Kheir  amewataka Vijana  kutengeneza programu endelevu Kwa  kujiendeleza kiuchumi kutokana na  Wafadhili kuanza kupungua  duniani .

Amesema kutokana  kupungua kwa Wafadhili wa Wakala wa Kimarekani  wa Msaada wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID)  hivyo ni vyema  Vijana kushirikiana kwa pamoja katika  Taasisi mbali mbali kwa kutengeneza  Programu ambayo itawasaidia  kupata kipato katika Kazi za staha kwa wote.

Akitoa Muhtasari wa taarifa za utekelezaji wa mwaka 2024 Hadi 2025  Mratibu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Zanzibar  Ndugu Salma Kombo Mohamed  amesemà jumla ya Vijana laki 325 Wamapatiwa mafunzo ya  Ujasiriamali na Uwezeshaji, Stadi za Maisha , Ushiriki na Ushirikishwaji , Afya ya Uzazi , Uongozi na Uzalendo, Mazingira ya Tabia ya nchi pamoja na Teknolojia na Mawasiliano .

Amesemà katika kitini Cha Stadi ya Maisha wameweza kutoa mafunzo Kwa Vijana 21 ambao walikuwa nje ya skuli na kutoa  mafunzo ya afya ya Uzazi Kwa Vijana 73,240 Kwa Unguja na Pemba .

Kwa Upande wa  Afisa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi Juma Rashid Ali akiwasilisha mada juu ya mambo muhimu kwa Vijana kuelekea Uchaguzi mkuu amesisitiza kutunza heshima nidhamu na maadili Kwa  kuachana na mihemko wakati wa Kampeni ,Uchaguzi na  kipindi cha matokeo ili kutunza  Amani na utulivu wa nchi .

"Vijana msikubali  kupokea vishawishi vyovyote vile ikiwemo kudhalilishwa na kutumika vibaya kwa kufanya vitendo  ambavyo vitapelekea  uvunjifu wa Amani,wala msitumie ya kijamii   kukashifu Viongozi ,msiombe wala kupokea rushwa msiharibu miundombinu iliyowekwa Kwa gharama kubwa ya Serikali ."alisema Afisa Uwezeshaji Juma Rashid .

Kwa Upande wa Vijana hao wameiomba Idara ya Vijana kuwapatia  mafunzo ya Fedha katika vikundi mbali mbali  ili kuweza kuwasaidia kukidhi sifa za kupatiwa mikopo na kumudu  kufanya marejesho.

Baadhi ya Vijana walioshiriki Kikao cha  robo  mwaka cha Uratibu  wa shughuli za Maendeleo ya Vijana Zanzibar.wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Shaib Ibrahim Muhamed (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Kariakoo,Wilaya ya Mjini .

Afisa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi Juma Rashid Ali akiwasilisha mada juu ya mambo muhimu kwa Vijana kuelekea Uchaguzi mkuu Kwa makundi ya Vijana katika Ukumbi wa Kariakoo,Wilaya ya Mjini .

Mratibu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Zanzibar  Ndugu Salma Kombo Mohamed akitoa Muhtasari wa taarifa za utekelezaji wa mwaka 2024 Hadi 2025  na muelekeo ya shughuli za maendeleo ya Vijana Kwa Mwaka 2025 hadi 2026 katika Ukumbi wa Kariakoo,Wilaya ya Mjini .
Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Ali Haji Hassan,  akifafanua juu ya Mabaraza ya Vijana kwa  Jumuiya Mbali mbali za Vijana (kushoto)  Muakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Idadi ya Watu ( UNFPA) na Masuala afya ya Uzazi . Amina Kheir na Mratibu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  Zanzibar  Ndugu Salma Kombo Mohamed katika Ukumbi wa Kariakoo,Wilaya ya Mjini .

Imetolewa na Kitengo Cha Habari.

WHVUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.