Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwaajili ya kufungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania leo tarehe 04 Juni 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) Mfamasia. Mavere Tukai wakati akikagua mabanda mbalimbali ya maonesho katika Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akisikiliza maelezo kutoka kwa Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Bw.
Boniface Magige kuhusu usimamizi wa maadili kwa wafamasia nchini wakati
akikagua mabanda mbalimbali ya maonesho katika Kongamano la Kisayansi na
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Paul Makonda pamoja na Viongozi mbalimbali, wakielekea katika Ukumbi
Maalum wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama
cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akikabidhiwa tuzo kutoka kwa Chama cha Wafamasia Tanzania mara baada ya Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano
Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 04 Juni 2025. (anayekabidhi tuzo ni
Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania Fadhil Hezekiah)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na Chama cha Wafamasia Tanzania kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na
maboresho katika sekta ya Afya. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Ufunguzi wa
Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania
unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo
tarehe 04 Juni 2025. (wanaokabidhi tuzo ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace
Magembe na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Paul Makonda)
No comments:
Post a Comment