Na Mwandishi Wetu. Dodoma
MWENYEKITI wa Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD), John Cheyo, amesema mchakato wa katiba unaendelea
vizuri na kwamba wakati walipozungumza na Rais Kikwete, walikubaliana uendelee
hadi likamilishe kazi ya kutunga katiba inayopendekezwa.
Akichangia kwenye bunge la
katiba jana, alisema ana imani kazi hiyo itakamilika katika kipindi hicho.
Akionekana kuwagusa moja kwa
moja UKAWA, Cheo alisema bunge hilo haliendeshwi kwa kelele za barabarani bali
linaendeshwa kwa sheria.
Alitaja sheria hiyo kuwa ni tangazo
la Rais katika gazeti rasmi la serikali (GN 254) ambayo inataja uhai wa bunge
kuwa unaishia Oktoba 4, 2014. Alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mfano wa kuigwa
katika kuleta suluhu ya jambo hilo.
Aidha alisema kila moja
alirekodiwa wakati wakizungumza katika majadiliano hayo, hivyo ameomba
zitengenezwe CD na kusambazwa ili Watanzania wajue viongozi wao walivyozungumza.
Aliwashangaa UKAWA kwa kupiga
kelele barabarani ilhali wakati wakizungumza na Rais Kikwete hawakuzungumza
wanayoyazungumza mtaani.
Alisema waliyoyazungumza kwa
waandishi wa habari ndiyo waliyokubaliana wakati wa mazungumzo na Rais Kikwete.
Alisema bunge la katiba lina
watu makini na aliwataka kujiamini ili
wakamilishe kazi zao kwa wakati.
Alisema kuna mambo mengi mazuri yamezungumzwa
kwenye bunge maalum hasa yanayowahusu wakulima, wafugaji na wavuvi.
Pia alisema suala la muungano
limepatiwa ufumbuzi ambapo Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na
Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Pili wa Muungano.
No comments:
Post a Comment