Na Mwanajuma Mmanga
WAISLAMU wanaokwenda kutekeleza
ibada ya hijja, wametakiwa kuwa na umoja na mshikamano ili kufanikisha ibada
hiyo.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh
Khamis Haji Khamis, alisema hayo wakati akifunga semina kwa Mahujaji hao Msikiti
Muwashawr Mwembeshauri.
Aidha aliwataka kutekeleza
masharti ya ibada hiyo ambayo inamuwajibikia kila Muislamu alie na uwezo.
Aliwataka viongozi wanaofuatana
na mahujaji kutekeleza wajibu wao ili mahujaji hao watekeleze ibada kwa
utulivu.
Kwa upande wa mahujaji, aliwahimiza
kuzingatia maagizo ya viongozi wao ikiwemo kuepuka kutembea pekee yao.
Sheikh Khamis aliwataka
wahudumu wa afya kuwasaidia mahujaji watakaopata matatizo wakati wakitekeleza
ibada hiyo.
Nae Katibu Mtendaji wa Umoja wa
Taasisi ya Hijja Zanzibar, (UTAHIZA), Ali Khatib Mranzi, alisema idadi ya
mahujaji wa Zanzibar inaongezeka kila mwaka.
Alisema lengo ni kupeleka
mahujaji 1,900 katika hijja ya mwaka ujao.
Hata hivyo, aliwataka Waislamu
wengine wenye uwezo kutekeleza ibada hiyo ambayo ni miongoni mwa nguzo tano za
Uislamu.
No comments:
Post a Comment