Na Madina Issa
RAIA wa Poland mwenye umri wa
miaka 31 (jina linahifadhiwa), anadaiwa kubakwa na mfanyakazi wake wa ndani.
Tukio hilo limetokea alfajiri
ya Septemba 14 katika kijiji cha Jambiaji Kibigija wilaya ya kusini Unguja,
ambapo mtuhumiwa ni mfanyakazi wa jikoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma
Sadi Khamis, amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni
Kantenina Alois Jakob (34) mkaazi wa kijiji hicho.
Alisema kabla ya tukio hilo,
mwanamke huyo aligombana na mume wake na kuamua kwenda kulala kwenye nyumba
nyengine.
“Siku ya tukio mwanamke huyu
aligombana na mume wake baada ya kurudi nyumbani wakitoka klabu ya starehe na
kwenda kulala nyumba nyengine, huku mume akiendelea kulala kwenye yumba yao ya
kawaida,” alisema.
Alisema mume alimjulisha
mfanyakazi wao kuhusu tukio hilo, lakini ilipofika usiku mtuhumiwa alikwenda
kwenye nyumba aliyolala bosi wake wa kike na kuingia ndani atakatekeleza
kitendo hicho.
“Alikuta mlango uko wazi,
akaingia ndani na akafanya kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali na
sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwa upelelezi,” alisema.
Alisema mwanamke huyo
alimefikishwa hospitali ya Makunduchi kwa matibabu na baadae kuhamishiwa hospitali
kuu ya Mnazimmoja.
Daktari wa kitengo cha mkono
kwa mkono hospitali kuu ya Mnazimmoja, Salum Omar Mbarouk, alikiri kumpokea mwanamke
huyo na kusema alipomfanyia uchunguzi aligundua michubuko kwenye sehemu zake za
siri na mikwaruzo ya kucha kwenye mapaja na kifuani.
Aidha alisema mtuhumiwa nae
alifanyiwa uchunguzi kwa kupimwa HIV na baadae kukabidhiwa jeshi la polisi
kuendelea na upelelezi.
Alitoa wito kwa wananchi
wanaofanyiwa vitendo vya udhalilishaji kuwahi kufika kituoni hapo ili kupatiwa
matibabu pamoja kutunza ushahidi utakaotumiwa wakati watuhumiwa wanapofikishwa
mahakamani,
No comments:
Post a Comment