Na
Husna Sheha
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk.Khalid Mohammed, amesema serikali inatafuta
vifaa vya kisasa kukabiliana na maafa.
Alisema
hayo wakati akizungumza na wanachama wa vyama vya siasa katika warsha ya
kukabiliana na maafa iliyofanyika hoteli ya 0ceaon View, Kilimani Zanzibar.
Alisema
serikali ya Zanzibar imeona umuhimu wa kuimarisha mikakati ya kukabiliana na
majanga ili maafa yatakapotokea athari yake isiwe kubwa kwa jamii na taifa.
Muhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Joseph Mayunga, aliwaasa wanasiasa
kuacha na utashi wa kisiasa na chuki na badala yake kuunda mpango mkakati wa
kukabiliana na maafa ili kuepusha majanga.
Aliwaomba
kuitoa taaluma waliyoipata kwa wanachama wao na kuwahimiza kutunza rasilimali
za nchi ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.
Nao
washiriki wa warsha hiyo, waliishauri serikali kujenga nyumba maalum ya
kuhifadhia maiti ili kuepusha usumbufu wakati majanga yanapotokea.
Warsha
hiyo ilitangulia na dua ya pamoja ya kuwaombea waliopatwa na maafa ya kuzama na
meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment