Na Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la
Katiba, Samuel Sitta, amesema baadhi ya nyaraka zinazosomwa makanisani ni
upuuzi mtupu na hazina utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Akiwakaribisha wageni waliofika
bungeni jana, ambao ni waumini wa dini ya kikiristu, Sitta, aliwataka wageni
hao kuwa waangalifu na baadhi ya nyaraka zinazosomwa makanisani kwa sababu ni
za kipuuzi na hazina utukufu wa Mungu.
Hivi karibuni Jumuiya ya
Kikiristo Tanzania (CCT) ilitoa waraka uliokuwa ukisomwa makanisani kupinga
Bunge Maalum la Katiba.
Akitoa idadi ya wajumbe wa
bunge hilo, Sitta, alisema idadi ya Wabunge wote wa Bunge Maalum ni 629, kati
ya hao idadi ya wabunge wa Tanzania Bara ni 419 na Zanzibar ni 210.
Aliseka akidi inayotakiwa kupitisha rasimu ya
katiba ni 280 kwa Tanzania Bara na 140 kwa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment