Na
Kauthar Abdalla
Hatimae wafanyakazi wa shamba la mipira la Kichwele wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja,
wameanza kulipwa mishahara yao baada ya kufanya kazi kwa muda wa zaidi ya miezi
sita.
Wafanyakazi
hao wamelipwa mishahara ya miezi miwili kuanzia jana.
Hata
hivyo, baadhi ya wafanyakazi hao wamegoma kuchukua mishahara hiyo na kusema
wataendelea na mgomo.
Wafanyakazi
hao walikuwa wamegoma kwa muda wa takribani mwezi mmoja, wakidai malimbikizo ya
mishahara yao.
Mwandishi
wa habari hizi, aliwashuhudia wafanyakazi hao wakilipwa, ambapo malipo
yalifanywa kwa mujibi wa siku ambazo mfanyakazi alizalisha.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi,Katibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Halima
Hussein Kuchilewa,alisema licha ya kuwa kampuni inazalisha kama kawaida lakini
wafanyakazi walikuwa hawalipwi mishahara yao kama kawaida.
Alisema
kitendo kilichofanywa na mwekezaji cha kutolipa mishahara, kimesababisha hali
ngumu za maisha pamoja na kushindwa kutunza familia zao.
Ofisa
kutoka Kamisheni ya Kazi Mkoa Kaskazini Unguja, Ame Haji Ali, alisema ni kweli Kamisheni
imepokea malalamiko ya wafanyakazi hao na imechukua juhudi za kuzungumza na
uongozi wa kampuni na ndipo walipokubali kuwalipa miezi miwili ya kwanza.
Alisema
licha ya baadhi ya wafanyakazi kumaliza mikataba, hakuna sababu ya kutolipwa
mishahara yao.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Sudi Mohammed Magumra, alisema tayari
ufumbuzi wa tatizo hilo umeshapatikana na fedha zilizosalia zitalipwa katika
kipindi cha mwezi mmoja ujao na kuwaomba wafanyakazi kurejea kazini.
Alisema
sababu kubwa iliyofanya mishahara kuchelewa ni upungufu wa uzalishaji na soko
la mpira katika viwanda vinavyonunua.
No comments:
Post a Comment