Na
Marzouk Khamis, Maelezo-Pemba
MKURUGENZI
Fedha wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC), Ismai Omar Bai, amesema
Shirika limepata mafanikio katika ununuzi na uimarishaji wa zao la karafuu
kutokana na ushirikiano inaoupata kuttoka kwa wakulima na wadau wa zao hilo.
Alisema
shirika litaendelea kugawa faida inayopatikana kutokana na zao hilo kwa
kusaidia maendeleo ya jamii kila hali inaporuhusu.
Aliyasema
hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo,Chake Chake katika
hafla maalum ya kukabidhi mashamiana kwa wajasiriamali wa soko la Jumapili
(Sunday Market) ambayo yametolewa na shirika hilo.
Alisema
ZSTC sasa imeelekeza nguvu zake kuisadi jamii katika shughuli za maendeleo
ikiwemo vikundi vya ushirika vya wajasiriamali na wakulima wa zao la kafaruu
kwa lengo la kuinua uchumi wao.
Alisema
miongoni mwa misaada inayotolewa na shirika hilo inaelekwezwa katika miradi ya
ujenzi wa barabara za vijijini ikiwemo ya Ngo'mbeni Mkoani na Kiwani, miradi ya
ujenzi wa skuli , biashara, umeme kwa vituo vya ununuzi wa karafuu na vikundi
vya ujasiriamali.
Mapema
akikabidhi mashamiana hayo kwa wajasiriamali hao, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,
Mwanajuma Majid Abdalla, aliwasisitiza kuyatumia vizuri na kulitumia soko hilo
kuendelea kibiashara.
Katiak
hafla hiyo Mkuu wa Mkoa alikabidhi mashamiana mawili yenye thamani ya shiling milion14.1.
No comments:
Post a Comment