Na Mwandishi wetu
SEPTEMBA
mwaka 2000, viongozi kutoka kote duniani walitia saini mkataba wa kutiumiza
Malengo nane ya kimaendeleo ya Milenia (Millennium Development Goals (MDG).
Kila lengo likidhamiria
kuimarisha maisha ya watoto wachanga kote ulimwenguni hasa kiafya, kielimu na
hata katika kutoa nafasi za kujiendeleza.
Lengo muhimu zaidi kati
ya haya ikiwa ni lile la kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaoaga dunia
kabla ya kufikisha miaka mitano.
Mahimbo Mdoe kutoka
Shirika la Kushughulikia Watoto (Unicef), anaelezea jinsi mataifa yanavyokazana
kutatua tatizo hilo.
Hatua
kadhaa zimechukuliwa lakini bado kunaendelea kushuhudiwa vifo vinavyoweza
kuzuiliwa.
Kwa mujibu wa Unicef,
mafanikio yanaendelea kupatikana katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto
wachanga, kwani kwa sasa idadi ya vifo vya watoto inaendelea kupungua kwa kasi
ya juu zaidi kuliko karne nyingine.
Hata hivyo, watoto zaidi ya milioni 6 hufa
kabla ya kufikisha miaka mitano hususan kutokana na sababu zinazoweza
kuzuilika.
Mataifa ya Afrika yaliyo
kusini mwa jangwa la Sahara ndiyo yaliyo na asilimia kubwa ya vifo ya watoto
wachanga wenye umri ulio chini ya miaka mitano.
Tangu 1990,MDG imekuwa
ikilenga kupunguza vifo hivyo kwa thuluthi mbili 2/3 kufikia mwisho wa mwaka
2015.
Majuma manne ya kwanza
tangu kuzaliwa kwa mtoto na hasa masaa ya kwanza ya kuwa duniani ndiyo hatari
zaidi.
Ingawa idadi ya watoto
wanaokufa katika muda huo imepungua, kasi yake imekuwa ndogo sana. Katika mwaka
wa 2003, watoto milioni 2.8 walikufa katika muda wa siku 28 toka kuzaliwa.

Lini lengo la Umoja wa
Mataifa litatimizwa?
Kati ya mwaka wa 1990 na
2003 watoto milioni 223 kutoka kote ulimwenguni walikufa kabla ya kutimiza
miaka mitano.
Idadi hii ni kubwa sana
hata kuliko idadi ya watu wote walio nchini Brazil.
Kwa mwendo huu, lengo la
kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa thuluthi mbili 2/3 halitotimizwa kabla
ya mwaka 2026.

No comments:
Post a Comment