Na Asya Hassan
OFISA Tawala wilaya ya magharibi,
Sabah Saleh, amesema kuanzishwa mabaraza ya watoto na wazee kutasaidia
kuimarisha maendeleo yao.
Alisema hayo katika uzinduzi wa
mabaraza hayo kwenye shehia ya Kiembesamaki katika hafla iliyofanyika viwanja vya sheha wa shehia hiyo.
Alisema kuwepo kwa mabaraza
hayo ni chachu ya kuwawezesha kujua haki zao pamoja na kuwajengea uwezo watoto
hao kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji yanayowakumba.
Alisema kumekuwa na matukio
mengi mabaya yanayofanywa kwa watoto na yanashindwa kufikia mwisho na kupata
haki zao za msingi.
Alisema kutokana na kukua
sayansi na teknolojia kunasababisha vijana kukumbwa na matukio mengi hali
inayosababisha kukosa haki zao.
Hata hivyo, Ofisa huyo alitumia
nafasi hiyo kuwataka wazee washirikiane na vijana wao katika kufanikisha maendeleo
ya mabaraza hayo na wasione kama watoto wao wanapewa mzigo.
Nae sheha wa shehia hiyo,
Mwinyi Khatib Juma, alisema watoto wamekuwa wakishawishiwa mara kwa mara juu ya
kujishirikisha katika makundi maovu hali inayopelekea kuacha maadili yao.
No comments:
Post a Comment