Na Joseph Ngilisho, Arusha
WANANCHI zaidi ya 24,000
waishio vijijini wanatarajia kunufaika na mradi wa umeme wa j na upepo katika
kipindi cha miezi 18 ijayo.
Hayo yalisemwa na Kamishana wa
Nishati na Petroli, Hosea Mbise, wakati akikagua maonesho ya makampuni 57 mkutano wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA)
jijini Arusha.
Alisema kikubwa katika mkutano
huo wanatarajia kuteuwa makampuni 20 kati ya hayo yalioshiriki maonesho hayo,
baada ya kushinda, ili wapewe kazi ya kusambaza umeme vijijini ambako gridi ya
taifa haipo.
“Umeme huo tunaamini utakuwa wa
bei nafuu kwa wananchi wengi wa vijijini na utawaondoa katika lindi la
umaskini,”alisema.
Aidha alisema makampuni
hayo ambayo yatateuliwa kwenye mkutano
huo, yataanza kazi mara baada ya kuteuliwa na ndani ya miezi 18 wananchi
watajionea umeme umesambaa kwa kasi maeneo yao.
Alisema gharama za mradi huo ni
shilingi bilioni 4.6, ambazo tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia makampuni
20 yatakayoshinda kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
“Fedha hizi zitagawanywa
kulingana na ukubwa wa kazi ya kampuni husika na kila kampuni itafanya kazi
katika kijiji chake ili mradi wasambae maeneo tofauti nchi nzima,” alisema.
Naye mmoja wa washiriki wa
maonesho hayo, Mkuu wa Idara ya Ufundi kwenye kampuni ya T&A Business
Center Ltd, Mgogiley Fivawo, alisema endapo kampuni yake itashinda atasambaza
umeme kwenye sekondari moja ya Rufiji na Vituo vya Afya viwili huko Rufiji.
Alisema eneo la Rufiji lina
rasilimali nyingi za uchumi kama zao la biashara la korosho, samaki na minazi,
lakini wananchi wengi hawana nishati ya umeme.
No comments:
Post a Comment