Na Madina Issa
MTU mmoja amefariki dunia baada
ya kufikishwa hospitali kuu ya Mnazimmoja, akipatiwa matibatu baada ya kugongwa
na gari.
Marehemu alitambulikana kwa
jina la Ali Faki Khamis (22) mkaazi wa Kinuni wilaya ya magharibi Unguja.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema
tukio hilo lilitokea Septemba 21 mwaka
huu saa 2:00 za usiku Amani.
Alisema kabla ya kifo,marehemu
alikuwa akiendesha baskeli maeneo ya Kibandamaiti kuelekea Amani na ndipo
alipopatwa na ajali ya kugongwa na gari yenye namba za usajili Z752 AG
iliyokuwa ikiendeshwa na Mbarouk Juma Khamis (53) mkaazi wa Amani.
Alisema marehemu alifikishwa
hospitalI kuu ya Mnazi Mmoja kwa kupatiwa matibabu na alipofanyiwa uchunguzi
aligundulikana kuwa alipata maumivu makali kichwani na kufariki dunia Septemba
22.
Hata hivyo, alisema katika
operesheni ya usalama barabarani katika mkoa wake kwenye wiki iliyopita makosa
207 yalikamatwa ambayo yanavihusisha vyombo mbalimbali vya moto.
Washitakiwa baadhi yao tayari
wameshapelekwa mahakamani na kesi zao
zimeshatolewa hukumu kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment