NAIROBI,Kenya
Msomi mashuhuri katika ukanda
wa Afrika Mashariki na dunia, Profesa Ali Mazrui, ameaga dunia nchini Marekani.
Mazrui raia wa Kenya alikuwa
msomi wa maswala ya kisiasa, utamaduni wa kiafrika na maswala ya dini ya
kiisilamu.
Mazrui aliyekuwa na umri wa
miaka 81 alifariki nchini Marekani ambako amekuwa akiishi baada ya kuugua kwa
mda mrefu.
Duru zinasema Prof.Mazrui
atazikwa mjini Mombasa Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Kabla ya kifo chake marehemu
Mazrui alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Binghamton mjini New York.
Kwa miaka mingi Mazrui alisikilizwa
na viongozi wa mataifa mengi ya Afrika na ya kigeni, akizungumzia nafasi ya
Afrika katika dunia nzima.
Alichapisha vitabu vingi na pia
kuandika nyaraka mbali mbali kuhusu siasa za Afrika, athari za siasa kwa dini
ya kiisilamu na uhusiano kati ya mataifa ya kaskazini na kusini.
Alipigia debe wazo la Afrika
kuwa huru na alikosoa mataifa yanayonyakua rasilimali za Afrika na kunyanyasa
watu wake.
Mapema mwaka wa1980, aliandika
na kutangaza makala kwa BBC yenye mada, 'The Africans - a Triple Heritage'
ambapo alionesha Afrika kuwa bara lenye mchanganyiko wa imani ya kiisilamu,
mfumo wa maisha ya kimagharibi na utamaduni asilia. (BBC News).
No comments:
Post a Comment