Na Mwanajuma Abdi, Dar es
Salaam
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, amesema kuna kila sababu ya kumuezi
hayati Mwalimu Nyerere, kwa kuwa alikuwa
ni kiongozi wa mfano katika bara la Afrika kutokana na busara zake.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa
alipofanya mahojiano na vyombo vya habari baada ya kumaliza mashindano ya
Rotary Dar Marathon, katika viwanja vya Osterbay.
Alisema Mwalimu wa Nyerere alikuwa mstaari wa mbele kudumisha amani na
kupinga ubaguzi wa aina yeyote.
Alisema ana kila sababu za
kumpongeza kiongozi huyo, ambae alimsaidia katika kumnyanyua hadi akapata
urais, jambo ambalo hakuwahi kulifikiria.
Alisema yeye alikuwa mwalimu kitaaluma
lakini Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mbunge na kumpa uwaziri mwaka 1970, jambo
ambalo lilisaidia kubadilisha maisha yake.
Alisema kitendo cha kumteua
kuwa waziri kilisaidia kumjenga kisiasa hadi kuwa Rais wa Tanzania.
“Mimi nilikuwa mwalimu
kitaaluma sikuwa na ndoto za kuwa Rais wa nchi hii, bali nilikuwa na mawazo ya
kugombania nafasi za kiongozi wa walimu
lakini yeye ndie aliyenisaidia kunifikisha hapa,” alisema.
Aliwapongeza viongozi wa klabu
za Rotary Dar Marathon kwa kuandaa mashindano hayo yenye lengo la kuleta
maendeleo katika nchi, ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 na vitu mbali mbali
vilikusanywa.
Mapema Mkuu wa Rotary kanda ya Tanzania
na Uganda, Harish Bhatt, alisema klabu sita za Rotary Dar es Salaam, zimeandaa
mashindano hayo, ambapo fedha zilizokusanywa zitatumika kwa ajili ya kujenga
kituo maalumu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment