Na Madina Issa
Idara ya Ustawi wa Jamii
Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar, imesema mtoto aliyetupwa
katika pwani ya Mawe matatu maeneo ya Migombani, anaendelea vizuri na kwa sasa
yupo nyumba ya kulelea watoto Mazizini.
Akizungumza na Zanzibar Leo,
Mkurugenzi wa idara hiyo, Halima Maulid Salum, alisema utaratibu wa idara ni
kukaa na mtoto kwa muda wa mwezi mmoja na kama atatokea mtu anaeaminika
akamtaka apewa.
Alisema tayari wameshajitokeza
watu wengi kumuomba mtoto huyo lakini idara inaendelea kuwachunguza ili mmoja
atakaekubalika apatiwe mtoto huyo kwa ajili ya kumlea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mjini
magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema mtoto huyo kwa sasa yupo chini ya
mikono salalama ya idara ya ustawi wa jamii.
Hata hivyo, alisema polisi wanaendelea
kumsaka mtu aliyemtupa mtoto huyo.
Mtoto huyo alitumwa akiwa
kwenya fuko la uzazi, tukio lililotokea Septemba 24 mwaka huu saa 11:00 jioni.
No comments:
Post a Comment