Na Joseph Ngilisho,Arusha
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon (18)
amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru, baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.
Tukio hilo la kusikitisha
limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 6.30 katika eneo la Tindigani,Kimandolu,wakati
mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika baa
hiyo kama mteja na baadae kumlazimisha mhudumu wa baa hiyo kufanya mapenzi bila ridhaa yake.
Simoni ambaye ni
mfanyakazi katika baa hiyo,
inayomilikiwa na Mwenyekiti wa mtaa, ,Joel Mbasha, alisema mnamo majira usiku
alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji na kumuhudumia.
Alisema ilipotimu majira ya saa
6.30 wateja waliisha na kuamua kufunga baa,hata hivyo mwanamke huyo alieendelea
kunywa pombe taratibu katika eneo la kaunta.
“Mimi sikuwa na mazoea kabisa
na mwanamke huyo kwanza ukimwangalia ni kama mama yangu,wakati nikifunga baa na
kujaribu kuondoka alinifuata na kuniambia anataka tukafanye mapenzi nilimkataa
ndipo aliponishika kwa nguvu sehemu zangu za siri,” alisema.
Alisema alipatwa na maumivu
makali na kuanza kupiga kelele ,ambapo mwanamke huyo aliendelea kumng’anga’nia
sehemu zake za siri huku akimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae
alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.
“Alipoona napiga kelele akaleta
mdomo wake kwenye mdomo wangu akanishika kichwa na kuniingizia mdomo wake huku
mkono wake mmoja ameshika sehemu zangu za siri nilikuwa nasikia maumivu makali
sana wakati nalia ndipo alipofanikiwa kuning’ata ulimi na kuondoka nao kisha
aliutema karibu na mlango wa baa,” alisema.
Majeruhi huyo kwa sasa hali
yake bado si nzuri kwani hawezi kuzungumza na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hali iliyosababisha wauguzi
katika hospitali anayotibiwa kumuwekea ndoo kutema damu.
Jeshi la polisi mkoani Arusha
limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi
utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment