Habari za Punde

Rais Kikwete anaendelea vyema na matibabu Marekani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini

Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.


Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. 

Tutaendelea kuwapatia taarifa ya maendeleo yake mara kwa mara. 

Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.

PICHA NA IKULU

1 comment:

  1. Taifa gani analolijenga kama kweli analijenga basi angetibiwa katika hilo taifa alolijenga, sasa wao wanakimbilia huko kwa matibabu, sisi walala hoi tunakufa hapa nyumbani hospitali hazina madaktari wanokijua wanachokifanya, hii ni aibu kubwa kwako muheshimiwa nchi unaongoza wewe, wewe ndio dhamana, kumbe unajuwa na unahakikishia watu kua huna unalolifanya,na sisi unotuongoza utufikirie tu , sisi hatuna uwezo wa kutibiwa huko, usipotufanyia mambo mazuri jua unabeba majukumu kwa Muumba, hayaa Mungu akupe nafuu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.