Askari wa usalama barabarani akiwa kazi katika mtaa wa mkunazi akilifungulia kesi daladala ya njia ya Bububu iliyokatisha safari yake na kushusha abiria wake jirani na kituo cha Mkunazini.
Kuna baadhi ya madereva wa daladala hawakamilishi safari za abiria wao wanaokwenda hospitali na kuwashusha njiani kama ilivyokuwa gari hii ikishusha abiria katika eneo hilo bila kujali shida za abiria hao kukatishwa safari yao.
Kuna baadhi ya madereva wa daladala hawakamilishi safari za abiria wao wanaokwenda hospitali na kuwashusha njiani kama ilivyokuwa gari hii ikishusha abiria katika eneo hilo bila kujali shida za abiria hao kukatishwa safari yao.
Safi sana askari kwa hili. Jambo hili kwa kweli linatuudhi mno sisi abiria. Pia nawashauri askari kukaa pale kituo cha melitano msikitini njia ya fuoni kuna tabia ya madereva wengi wa njia ya Fuoni hawawafikishi abiria mwisho Wa kituo yaani Fuoni Polis I bad ala yake huishia safari zao hapo melitano msikitini. Tabia hii pamoja na kwamba kinyume taratibu Bali pia maudhi name keep kubwa kwa abiria. Lengo kubwa la kufanya suala la usafiri kuwa sekta binafsi ni kuwasaidia wananchi kujiajiri wenyewe na kupunguza tatizo la ajira lakini kuna baadhi ya madereva wanajifanya wababe mno. Nashauri askari mulifanyie kazi suala hili daladala zote zisizowafikisha abiria mwisho Wa kituo kilichopangwa basi madereva wake wanyang'we kabisa leseni zao za udereva na magari hay yazuiliwe kabisa kufanya kazi za kusafirisha abiria.
ReplyDeleteNaungana na mdau hapo juu. Hii tabia imekithiri mno rout ya Fuoni. Utamsikia kondakta akiwa Michenzani ananadi Mwisho Fuoni Melitano wakati rout yake inaishia Fuoni Polisi. Askari kama mtafanya kazi kwa umakini basi mtawanasa madereva wengi wenye kukiuka taratibu za kazi ya usafirishaji. Madereva wengi pamoja na makondakta wao ni watu wasio na maadili na ustaarabu Wa kuwahudumia abiria. Nashauri wakati mwengine askari muingie hasa kernye daladala bila kujulikana (bila uniform) ili kuwakamata kirahisi hawa wasiofuata taratibu.
DeleteMadereva wengi Wa daladala mbali na tamaa kubwa ya kupata pesa lakini hata mahesabu yao ovyo kabisa. Utamkuta konda anaongeza abiria 2 kwa shilingi 600 huku akijua akishikwaa atatoa 5000/ Huu ni ujinga na kwa siku anaweza kupigwa 'mbungo' Mara kadhaa kwa hiyo sometime wanakosa faida kwa makosa ya kijinga kabisa. Madereva Wa daladala jirekebisheni na mheshimu kazi zenu.
ReplyDeleteSerikali inapaswa nayo ijitathmini kuhusu suala la kubinsfsisha moja kwa moja sekta ya usafirishaji baharini name nchi kavu. Bado wamiliki Wa vyombo pamoja na watendaji wao hawawathamini kabisa abiria yaani hakuna kabisa kile kitu kinaitwa costumer care hasa katika madaladala. Mbali na tatizo alozungumza mdau Wa kwanza kuna tatizo jengine linaanza kujitokeza Zanzibar nalo ni la wanafunzi kutokuchukuliwa kwenye daladala hasa nyakati za asubuhi. Serikali inapaswa kuwaangalia kwa kina kwa maslahi ya abiria na we ye Mali.
ReplyDeleteKuna tatizo pia kwa daladala ziendazo Chuo Kikuu Tunguu kutokuwachukua abiria wanaoshuka Fuoni. Mimi hushangaa Gari inakwenda Tunguu kupitia Fuoni lakini abiria Wa Fuoni hachukuliwi?? Askari naomba na hili mlifanyie kazi. Kuna kadhaa Wa kadha kwenye madaladala kama mkichakarika vizuri basi inaweza kupata fedha nyingi (faini) kwa madereva wazembe au wahuni au wababe. Mdau Fuoni.
ReplyDeleteMimi nashauri askari wakafanya survey na wakakusanya matatizo mbalimbali yabayojitokeza kwenye usafiri Wa daladala kisha wakaandaa mtaala (curriculum) special kwa ajili ya madereva na makonda Wa gari za abiria. Then kila Dereva na konda wa daladala ni lazima apite kwenye kwenye Mafunzo hayo maalum kwa ajili yao asipita huko asipewe leseni ya kuwa Dereva wala konda Wa gari za abiria. Lakini LAZIMA tuwe serious katika hili maana watanzania tunajuana kwa 'short cut'.
ReplyDeleteMadereva wengi kwa kweli ni unqualified kufanya hizi kazi. Utamuona Dereva kafungua radio anasikiliza muziki ndani ya daladala kwa sauti kubwa kubisa utadhani labda ni ukumbi Wa disco. Ndani ya gari kuna wagonjwa wala hajali ukimwambia jeuri juu kwa juu. Kwa kweli askari kuna mengi maovu ndani ya madaladala yanayopaswa kushughulikiwa. Usafiri huu umekuwa ukionekana Wa kihuni zaidi kuliko ustaarabu kutokana na tabia chafu za madereva na wasaidizi wao.
ReplyDelete