Kipa wa timu ya Mtibwa Sugar Said Abdallah akiwa kenda ola wakati wa upigaji wa penenti katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Simba imeshinda kwa penenti 4--3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Bi Shery Khamis akiongozana na Rais Shein kwenda kukabidhi zawadi kwa washindi wa Kombe hilo.mchezo uliofanyika uwanja wa amaan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Mbarouk, kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Bi Shery Khamis, Rais wa ZFA Ravia Idarous na Rais wa TFF Ndg.Jamal Maliz wakiwa katika jukwaa la kukabidhi zawadi kwa washindi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waamuzi waliochezesha mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Mtibwa Sugar, uliofanyika katika uwanja wa Amaan, timu ya Simba imeshinda kwa penenti 4--3.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwavisha nishani washindi wa Pili wa Kombe la Mapinduzi timu ya Mtibwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi fedha Nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar, zawadi ya mshindi wa pili fedha taslim.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimvisha Nishani ya Dhahabu kipa wa timu ya Simba Mapunda.baada ya timu yao kuibuka Bingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kocha Mkuu wa timu ya Simba Gorad baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Fainali na timu ya Mtibwa Sugar. na kushinda kwa penenti 4--3.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi fedha Nahodha wa timun yac Simba, baada ya timu yake kunyakuwa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2015. kwa kuishinda Mtibwa Sugar kwa penenti 4--3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Shery Khamis akimkabidhi Kombe la Bingwa wa Kombe la Mapinduzi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, ili kulikabidhi kwa Bingwa wa michuano hiyo timu ya Simba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Mapinduzi Cup nahodha wa timu ya Simba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Mapinduzi na Wachezaji wa Timu ya Simba baada ya kuwakabidhi kombe lao la Ubingwa wa Mapinduzi Cup.
Kikosi kazi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja na Kombe lao la Ubingwa wa Mapinduzi Cup.
No comments:
Post a Comment