Habari za Punde

Doris Mollel Foundation yazinduliwa jijini Dar

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
TATIZO la Vifo vya watoto njiti limezidi kukua kutokana na kukosekana  kwa vitendea kazi katika vituo vya kutolea hudum za afya.

Hayo ameyasema, Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo wakati wa kutambulisha Mfuko wa Doris Mollel ambao  utajihusisha katika kusaidia upatikanaji wa vitendea kazi vya hospitali  kwa watoto wanaozaliwa njiti iliyofanyika  katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.amesema atatoa ushirikiano wa kutosha kwa mfuko huo huku akiutaka uende pia Zanzibar na kukutana Baraza la wawakilishi.

Kombo amesema Mollel amejitambua na ana umuhimu wa kusaidia watoto njiti  kutokakana na kutambua alikotokea na matatizo gani wanayokumbana nayo watoto njiti.

Mwenyekiti wa Mfuko huo ,Doris Mollel ambaye Mrembo wa Singida 2014/15,amesema yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2  na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.

Amesema lengo la mfuko ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia jamii katika upande wa watoto njiti ambapo takwimu zilizopo zinaeleza idadi ni ndogo kutokana na jamii nyingine hazina utamaduni wa kwenda kujifungulia katika vituo vya afya hivyo elimu inahitajika kufanya jamii hizi zifike katika vituo vya afya na kuwezeshwa kwa vituo hivyo kuwa na vifaa na kuweza kupunguza vifo hivi kutoka 9000 hadi 1000 au kuondoa kabisa.

Doris amesema takwimu zinaonyesha kuwa watoto 213,000 wanazaliwa wakiwa njiti na 9,000 wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya vifaa vya kufanya  waweze kukua katika joto linalostahili.

Kwa upande wa Balozi Mwanaidi Maajah amesema kuwa Doris amejitoa katika kusaidia upande wake aliotokea kwa kutambua kuwa kuna mchango unahitajika katika kusaidia watoto wanaozaliwa wakiwa njiti.

Katika hafla hiyo watu mbalimbali wamechangia ambapo fedha tasilim sh.800,000 zimepatikana na ahadi ni sh. ya Milioni 4.7.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.