Uongozi wa Jumuiya ya Baraza la Maulid Tomondo Zanzibar (blmt),
ukishirikiana na ofisi ya Mufti Zanzibar pamoja na Taasisi za Kiislamu,
unawatangazia na kuwaomba waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuhimizana
kuhudhuria katika shughuli ya dua maalum ya kitaifa ya kuiombea nchi yetu itakayojumuisha
Maulid ya bwana Mtume Muhammad (S.A.W), itakayofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 21 Machi 2015 kuanzia saa moja (1)
usiku hadi saa tano (5) usiku katika uwanja wa Amaan Stadium mjini Zanzibar.
Sala za Magharibi na Isha zitasaliwa kwa nyakati zake na kwa jamaa kubwa
hapo hapo uwanjani.
Shughuli hii ambayo ni kwa ajili ya wanaume tu itahudhuriwa na wanazuoni
mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu, waheshimiwa viongozi wetu wa
kiserikali, asasi za kiraia, wafanyabiashara n.k.
Vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwepo kusimamia amani na utulivu wa
shughuli hio mwanzo hadi mwisho.
Milango ya viwanja vya Amaan itakuwa wazi kuanzia saa kumi na mbili (12
) za jioni
Waumini nyote mnakaribishwa, shime shime shime tuhudhurieni kwa wingi
sana tukamuombe Mwenyezi Mungu amani kwa ajili ya visiwa vyetu.
Usafiri wa mashamba ng'ambo na mijini utakuwepo in shaa Allaah
No comments:
Post a Comment