Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuika na Viongozi na waislamu katika kisomo cha Hitma ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishiwa Jimbo la Magomeni (CCM) iliyosomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri Mjini Unguja hitma hiyo ilihudhuriwa na Waumini na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Waislamu na Viongozi mbali mbali na wananchi wakiwa katika kisomo cha Hitma ya kumuombea Dua Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni Hitma hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawar Mwembeshauri,[Picha na Ikulu.]
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitoa mawaidha baada ya kisomo cha Hitma ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilichi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni Hitma hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri,[Picha na Ikulu.]
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa shukurani kwa Viongozi mbali mbali Waislamu na Wananchi na wapenzi wa CCM baada ya kisomo cha Hitma Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilichi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja iliyosomwa leo katika Msikiti wa Mushawal Mwembesahauri Marehemu alifariki hivi karibuni na kuzikwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.] ]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 1.3.2015
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na viongozi mbali mbali wa dini,
vyama na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar
katika hitma ya kumuombea marehemu Salmin Awadh Salmin aliyekuwa Mwakilishi wa
Jimbo la Magomeni
Hitma hiyo
iliyotayarishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM )Zanzibar, ilisomwa katika Masjid
Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar na kutanguliwa na Qur-an Tukufu iliyosomwa na Sheikh Sharif
Abdulrahman.
Viongozi wa dini
nao walipata fursa ya kutoa mawaidha kwa mnasaba wa tukio hilo ambapo Katibu
Mkuu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga alitoa mawaidha juu ya mada inayohusu mauti
pamoja na haja ya kumuombea dua maiti.
Aidha, Sheikh
Soraga alitumia fursa hiyo kutoa visa mbali mbali vya Masahaba juu ya mauti
kikiwemo kisa cha mauti yaliyomfika Bwana Mtume Mohammad (S.A.W).
Nae Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alitoa shukurani kwa viongozi wa dini,
vyama vya siasa na Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria katika Hitma hiyo.
Naibu Vuai
alisema kuwa Marehemu Salmin Awadh mauti yamemchukua akiwa katika shughuli za
kuimarisha Chama Cha Mapinduzi huko Kisiwandui mjini Zanzibar, Sambamba na
hayo, Naibu Vuai alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Alhaj Dk. Shein kwa
faraja zake kwa viongozi alizozitoa juu ya msiba huo.
Miongoni mwa
viongozi waliohudhuria ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, Mawaziri, Wabunge,Wawakilishi na
viongozi wengine wa Serikali, dini na vyama vya siasa pamoja na wananchi kutoka
Mikoa ya Unguja Kichama na Kiserikali.
Rajab
Mkasaba, Ikulu
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
No comments:
Post a Comment