Habari za Punde

Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Yazindua Kituo cha Upimaji wa Usikivu wa Watoto Wachanga

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.   
Waziri wa Afya wa Zanzibar,Mhe.Rashid Seif Suleiman amesema sikio,  mdomo  na macho ni sehemu muhimu sana katika maisha ya  binaadamu hivyo unapokuwa na   wataalamu wa  kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa kuenziwa.

Haya ameyasema jana katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi  wa kuwapima usikivu watoto wachanga mara  baadaya kuzaliwa ili kujua matatizo yao.

Amesema uchunguzi  wa watoto wachanga kujua usikivu wao  mapema ni mpango mzuri  ambao utalisaidia Taifa kuwa na   watoto wenye usikivu  mzuri na njia rahisi  ya kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.

“Kujua tatizo la kiafya mapema na kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za matibabu hivyo nawanasihi wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya kujifungua, ”alisisitiza Waziri wa Afya.

Amesema  maradhi ya usikivu  yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo kila mzazi atatimiza wajibu wake wa kumpeleka  mtoto wake  kupata vipimo yataweza kupungua.


Waziri wa Afya aliwataka wazazi  kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali  ili kupata huduma hiyo kwa urahisi na watakaozalia majumbani  kuwapeleka watoto wao kuchunguzwa usikivu mara baada ya kuzaa.

Aidha Waziri huyo aliwataka madaktari  waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto wachanga  na wazazi zinahitaji uvumilivu.

Waziri alisema tatizo la uskivu huazia  mtoto  anapochelewa kulia mara baada ya kuzaliwa ama wanapopata homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi kuchelewa kuzaa baada ya uchungu wa muda  mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya ya kufika muda wa kuzaliwa.

Nao madaktari walio patiwa mafuzo hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa kuwapima usikivu watoto  na kubaini matatizo yao  na kuishauri Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.

Mradi huo wa kupima watoto usikivu ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka Jumuiya ya Madaktari wanotoa huduma za matibabu vijijini ( ZOP) ambavyo vina thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.